Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 16, 2012

AMIR KHAN AKATALIWA 'KUMREJEA' KOCHA Freddie Roach



LONDON, England

SIKU moja tangu alipotangaza kuachana na mkufunzi wa Freddie Roach, bondia Amir Khan amefanya jaribio la kumrejeshea wadhifa wake kocha huyo, ikiwa atakubali kumtanguliza mbele ya mabondia Manny Pacquiao na Julio Chavez Junior anaowanoa pia.

Lakini Roach amelikataa jaribio hilo mara mbili, ambapo awali alipigiwa simu na Khan, kabla ya Mwingereza huyo kukutana uso kwa uso na kocha wake kumuomba kwa mara ya pili.

Roach alithibitisha hayo alipoongea kutoka Los Angeles, Marekani anakoishi na kusema: “Wao waliniambia kama nitampa kipaumbele Amir, na kisha wafuate Manny na Chavez, watakubali kunirudisha katika kambi yao.

“Yote niliyakataa na nikawaambia hapana, siwezi kufanya hayo,” alifichua Roach, mkufunzi aliyejizolea umaarufu nchini Marekani na duniani kwa ujumla.

Habari za ndani ya kambi ya Khan, zimefichua kwamba, Bernard Hopkins amependekeza Nazeem Richardson kuwa mbadala wa Roach katika jukumu la kumpa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...