Mwenyekiti
wa Chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania, TASWA, Juma
Pinto, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo, katika
Mgahawa wa City Sports Lounge, alipokuwa akiwatambulisha baadhi ya
wasanii watakaotoa burudani siku ya Bonanza hilo, (kushoto kwake) ni
Menjea Mawasiliano wa TBL, ambao ni wadhamini wakuu wa Bonanza hilo,
Doris Malulu, Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki na
wanamuziki wa bendi hiyo, wakiongozwa na Super Nyamwela.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo, wakiwa bize kunakili kinachozungumziwa.
Baadhi ya wanenguaji na wanamuziki wa bendi hiyo, waliohudhuria mkutano huo leo.
Wanahabari wakiwa bize kunasa matukio katika mkutano huo leo
Mkurugenzi
wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, akifafanua jambo kuhusu maandalizi
ya bendi yake katika Bonanza hilo, wakati wa mkutano huo leo.
*********************************
Na Mwandishi Wetu
BENDI
ya muziki wa dansi ya Extra Bongo na kundi la taarabu la Jahazi Modern
ndiyo burudani zitakazonogesha tamasha la vyombo vya habari
litakalofanyika Dar es Salaam kesho (Jumamosi).
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mchana katika Mgahawa
wa City Sports Lounge, wakati wa kutambulisha burudani hizo, Mwenyekiti
wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)
kinachoandaa bonanza hilo, Juma Pinto, alisema maandalizi kuhusiana na tamasha hilo linalojulikana kama Media Day Bonanza yamekamilika.
Alisema
wameichukua Extra Bongo inayoongozwa na Ally Choki na Jahazi Modern
inayoongozwa na Mzee Yusuph kutokana na makundi hayo kuwa juu hivi sasa
katika muziki kwa maeneo yao.
“Tunaamini
watakaokuja kwenye tamasha watakuwa na furaha ya aina yake na
tumejiandaa vya kutosha,” alisema Pinto na kueleza kuwa bonanza hilo
litafanyika viwanja vya Sigara Chang’ombe, Dar es Salaam na mgeni rasmi
atakuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
Pia
Pinto alisema bendi ya Msondo Ngoma Music itapiga kwenye viwanja hivyo
kuanzia saa moja usiku baada ya bendi za Extra Bongo na Jahazi kumaliza
kutumbuiza Media Day na kwamba imetoa ofa kwa wanahabari watakaotaka
kubaki kuendelea kupata burudani mpaka usiku wa manane.
“Msondo
wana bonanza lao kila Jumamosi, sasa wamekubali kwamba wanahabari
watakaotaka kubaki baada ya bonanza kumalizika jioni wabaki wajiunge na
Msondo Ngoma,” alisema Pinto.
Bonanza
hilo la TASWA linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) likiwa na
lengo la kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa
siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa
vyombo mbalimbali vya habari ili kubadilishana mawazo na kufurahi
pamoja.
Kwa
upande wake Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu alisema wamejipanga vya
kutosha na kwamba wadau wafike kwa wingi kuhakikisha mambo yanaenda
kama yalivyopangwa.
“TBL
ni mdau mkubwa wa wanahabari, tumewaandalia mambo mazuri, naomba
msikose,” alisema Malulu na kuongeza kuwa wanaamini wadau 1,500 kutoka
vyombo mbalimbali vya habari wanaotarajiwa kushiriki bonanza hilo
watafurahi vya kutosha siku hiyo.
Naye
Choki akizungumza kwenye mkutano huo, alisema vijana wake wamejipanga
vya kutosha kushambulia na kuwa dhamira yao ni kuona wana habari
wanafurahi vya kutosha na kuwa mambo waliyowaandalia kila mtu atafurahi
kuiona Extra Bongo.
No comments:
Post a Comment