Na Elizabeth John
MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya
nchini ambaye anauwakilisha mkoa wa Morogoro, Seleman Msindi ‘Afande Sele’
ameachia albamu yake mpya inayojulikana kwa jina la ‘Amani na Upendo’.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam leo, alisema licha ya soko la mauzo ya
albamu kusuasua hatojali mauzo mabaya kwakuwa lengo lake ni
kuelimisha jamii na sio kupata maslahi.
“Sitofikilia soko kama
litalipa au vipi ninachohitaji ni kuwapa elimu watanzania, mashabiki wategemee
kununua albamu hiyo kwa bei rahisi,” alisema.
Alisema anaomba mashabiki waipokee
vizuri kazi hiyo na kwamba ina jumla ya nyimbo 10 ambazo zote zimefanya vizuri
katika soko hilo.
No comments:
Post a Comment