Mkurugenzi
wa Hoteli ya Sapphire Court ya Jijini Dar es Salaam, Abdulfatah Salim
(kulia) akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo, Nahodha wa timu ya
wamiliki wa Magazeti 'Tando' Blogers Fc, Muhidin Sufiani, ambaye ni
mmiliki wa mtanda wa www.sufianimafoto.com, kwa ajili ya kushiriki
katika Bonanza maalum la waandishi Medi Day linalofanyika kwenye Viwanja
vya Leaders Club Kinondoni kesho. Katikati ni Meneja wa muda wa timu
hiyo, Mroki Mroki. Timu hiyo ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza katika
michezo na bonanza kama hilo, inatarajia kushiriki katika michezo yote
itakayo chezwa hiyo kesho, ikiwa ni pamoja na Soka, Netiboli, Kukimbiza
Kuku, Kukimbia na Magunia, Kuvuta Kamba, Kucheza Pool, Kuimba na Kudansi
'Sebene' na mingineyo.
Makabidhiano yakiendelea, hii ni Jezi ya Kipa.
Nahodha
wa timu hiyo Sufianimafoto (kushoto) akiwa na Meneja wa muda wa timu
hiyo, Mroki Mroki, wakiwa na Vifaa vilivyokabidhiwa.
Na Mwandishi Wetu
HOTELI ya Sapphire Court iliyopo makutano ya
mitaa ya Swahili na Lindi, Dar es Salaam leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa
timu ya wamiliki wa magazeti tando (Blogers FC) kwa ajili ya Bonanza la Media
Day, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni,
Dar es Salaam.
Akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Sapphire,
hoteli iliyojizolea umaarufu mkubwa kwa sasa nchini, Abdulfatah Salim Saleh
amesema ameamua kukabidhi vifaa hivyo ili kuunga mkono timu hiyo mpya
inayoanzishwa katika tasniya ya michezo nchini.
“Nilipopata ombi lenu, sikutaka hata kujifikiria,
nilisema nitawasadia, na huu ni mwanzo tu. Naahidi kushirikiana nanyi zaidi na
zaidi na ninawakaribisheni wakati wowote, mimi ni shabiki wa timu yenu kuanzia
sasa,”alisema.
Kwa upande wake, Meneja wa Muda wa Blogers FC,
Mroky Mroky alisema kwamba wanashukuru kwa msaada huo na wanaahidi kudumisha
uhusiano mzuri na Sapphire.
“Wazo hili la kuanzisha timu ni la muda mrefu,
lakini lilikuwa likisuasua, ila tukaamua kwa vyovyote lazima tutokee kwenye
Media Day ya mwaka huu. Tulipofikiria suala la wapi tutapata vifaa vya michezo,
vichwa vilituuma kidogo, lakini tunashukuru Sapphier wametuliza maumivu
hayo,”alisema Mroky.
Naye Nahodha wa Blogers FC, Muhiddin Sufiani
amesema kwamba baada ya kupata vifaa hicyo kesho wanatarajia kuanza kuonyesha
cheche zao kesho katika Bonanza la Media Day, lengo likiwa ni kubeba ubingwa
upande wa soka na kutwaa pia mataji mengine madogo madogo.
Miongoni mwa wachezaji nyota wanaotarajiwa
kuichezea Blogers FC kesho ni Issa Michizi, Majjid Mjengwa, Sufiani mwenyewe,
Majuto Omary, Joseph Lukaza, Shaffi Dauda, Saleh Ally, Mahmoud Zubeiry, Millard
Ayo na John Bukuku.
Bonanza la wanahabari linaloandaliwa na Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), litafanyika kesho kwenye
viwanja vya Leaders, chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Pamoja na wanahabari kuchuana katika michezo
mbalimbali, lakini Bonanza hilo pia litapambwa na burudani ya bendi ya Extra
Bongo na kundi la taarabu la Jahazi Modern.
Kutakuwa pia na mechi maalum baina ya wanahabari
ambao wameoa na wale ambao hawajaoa utakaofanyika baada ya michezo ya kawaida
baina ya vyombo vya habari kumalizika.
No comments:
Post a Comment