Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 4, 2013

HUDUMA YA BANDO NA TTCL YAZINDULIWA LEO


 Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akionesha aina mpya ya Smart Phone wakati wa uzinduzi wa Huduma ya Bando na TTCL na kampeni ya punguzo kubwa la bei ya intaneti uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mauzo TTCL, Kisamba Tambwe. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akizindua Huduma ya Bando na TTCL na kampeni ya punguzo kubwa la bei ya intaneti uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Bidhaa TTCL, Issaya Ernest.


KAMPUNI ya simu Nchini (TTCL) leo imezindua huduma mpya ya  Bando na TTCL  itakayomuwezesha mteja kufaidika na meseji  bila kikomo ,kuperuzi intaneti  na muda wa maongezi kwenda mitandao yote kwa bei nafuu.

DAR ES SALAAM, Tanzania

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kaimu  Ofisa Mkuu wa Mauzo Peter Ngota alisema huduma ya bando na TTCL itamuwezesha mteja pia kutuma meseji bila kikomo kwa bei ya hadi shilingi mia tano.
Alisema bando TTCL inawalenga zaidi watumiaji wa simu za kisasa za smart phones za kampuni hiyo ambazo zinapatikana katika vituo vyao vya simu kote nchini.

Alisema kampuni hiyo imeshusha kwa kiwango kikubwa bei ya vifurushi vyake vya mobile internet kwa kampeni ya Basti ikimaanisha peruzi internet zaidi kwa gharama nafuu.

“Hii ni punguzo la bei la aina yake , mathalani kifurushi cha mwezi cha 4GB kilichokuwa kinauzwa  shilingi 90,000 sasa kinauzwa  shilingi 25,000 hii ni nafasi sit u kwa wateja waliopo TTCL kuongeza matumizi kwa gharama nafuu bali hata kwa wateja wapya ikiwamo watumiaji wadogo kujiunga  na mtandao wa TTCL,”alisema Ngota.

Alisema Bando na TTCL  na kampeni ya Basti zina manufaa kkwa mteja ikiwa ni pamoja na huduma ya mobile internate kwa gharama nafuu,vifurushi vya siku ,wiki na mwezi kulingana na mahitaji ya mteja,mobile internate yenye ubora na kasi ya juu zaidi,kwa kununua modemu ya shilingi 29,900 utapata 2GB bure kuperuzi intaneti.

Aidha alisema kua huduma ya bando na TTCL inapatikana pia kwa simu za kisasa za smart phones na inatoa thamani bora kwa pesa  huku akieleza kua kama kampuni kongwe na mhimili wa mawasiliano nchini inatambua kuwa na jukumu kubwa la kutoa huduma za mawasiliano kwa wateja kote nchini.

1 comment:

  1. ttcl bado mnababaisha,alafu ni aibu kwa kampuni kongwe kama hiyo,huduma zenu ni gali sana zinatushinda,mimi nilikuwa na mordem ya ttcl lakini nimelazimika kununua tena airtel,achilia mbali garama zenu lakini hata coverage yenu ni mbovu sana,mmelaza sana mmekuwa kama tritel na mobitel enzi zile wakidhani biashara ya mawasiliano iko miji mikubwa,angalia airtel tshs.1999 unapata dakika 70 kwenda mitandao yote kwa wiki, 175mb na 700sms hivi kweli nitaacha offer kama hiyo nifuate offer ya 25,000 ambayo mwanzo ilikuwa 90,000,mnategemea nini.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...