CHAMA cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),
kimetangaza kuanza kwa Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam, hatua ya sita
bora.
Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo, amesema hayo leo
Aprili 5 kuwa ligi hiyo itaanza Aprili 9 mwaka huu hadi 31 katika viwanja
vitatu vya Shule ya Sekondari Benjamin
Mkapa, Kinesi na Makurumla.
Alizitaja timu zitakazochuana katika hatua hiyo kuwania kucheza
Ligi ya Kanda Taifa kuwa ni pamoja na Boom FC ya Ilala, Friends Rangers ya
Magomeni, Abajalo FC ya Sinza, Red Coast ya Mburahati, Day Break ya Magomeni na
Shariff Star ya Ilala.
“Kwa mujibu wa ratiba yetu, kila siku kutakuwa na mechi
tatu, hivyo katika mechi za ufunguzi Aprili 9, Boom FC wao watachuana na
Shariff Star, kwenye Uwanja wa Airwing, wakati Day Break watamenyana na Friends
Rangers uwanja wa Makurumla huku Red Coast wao watacheza dhidi ya Abajalo,”
alisema Mharizo.
Timu tatu katika ligi hiyo zitawakilisha mkoa katika Ligi ya
Kanda Taifa hapo baadae.
Wakati huo huo, Mharizo amesema kabla ya kaunza kwa ligi
hiyo, kutatolewa semina elekezi kwa viongzi wa timu shiriki, itakayofanyika
Jumapili kwenye Ukumbi wa Shule ya BenjaminMkapa kuanzia saa nne asubuhi.
“Lengo la semina hii elekezi ni kutoa elimu kwa viongozi na
wachezaji ili kuondoa mvutano wakati wa ligi hiyo, nia yetu ni nzuri na
tunapenda kuona ligi ikichezwa kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa,”
alisema Mharizo.
Semina hiyo itawahusisha Katibu, Mwenyekiti, Kocha, Nahodha
na Waamuzi 16 watakaochezesha ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment