Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, February 21, 2014

KALAMA NYILAWILA ASAINI MKATABA WA KUCHEZA NA BINGWA KATI YA MASHALI AU KASEBA MEI MOSI


Bondia Kalama Nyilawila katikati akitia saini ya kucheza pambano siku ya mei mosi atacheza na Thomasi Mashali au Japhert Kaseba inategemea na mshindi wa mechi hiyo ya March 29 itakayofanyika PTA Sabasaba kulia ni Alli Mwazoa na Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Promota wa ngumi nchini Ali Mwazoa akipeana mkono na Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi baada ya kumsainisha bondia Kalama Nyilawila katikati anaetarajia kuzipiga mei mosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Promota wa ngumi nchini Ali Mwazoa akipeana mkono na Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi baada ya kumsainisha bondia Kalama Nyilawila katikati anaetarajia kuzipiga mei mosi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu

Bondia Kalama Nyilawila Ameingia mkataba wa makubaliano na promota Ali Mwazoa wa Tanga kwa ajili ya mpambano wa Mei Mosi mwaka huu ambapo  anasubili mshindi wa mpambano kati ya Thomasi Mashali na Japhert Kaseba ambao watazichapa March 29 katika ukumbi wa PTA Sabasaba ambapo mshindi atacheza na

Kalama Nyilawila siku ya  mei mosi akizungumza baada ya kusaini mkataba huo bondia Kalama Nyilawila alijitapa kwa kusema iwe Mashali awe Kaseba yoyote atakae kutana nae ato kuwa na masiara nae atampiga kipigo cha mbwa mwizi kwani nafasi hiyo alikuwa anaitafuta siku nyingi baada ya kupoteza huwezo wake katika masumbwi hivyo sasa wakae mbali na mimi kwani nakuja kwa nguvu mpya kabisa akisema atakuwa hatari kama 'Mbeya City' timu ambayo inatoka mkoani kwao na kufanya maajabu kwa kuitawala ligi kuu ya Tanzania bara ndivyo na mimi nitakavyofanya

Kalama katika harakati zake za kuhakikisha anarudi katika chati kama zamani mechi yake ya mwisho katika kuukaribisha mwaka 2014 alimsambalatisha bondia Ibrahimu Maokola bila huruma kwa kumpiga K,o ya raundi ya pili mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Msasani klabu

Nae promota wa mpambano huo Mwazoa amesema kila kitu kinaendelea vizuri ikiwemo mapambano ya utangulizi yenye mabondia bora wanaotamba kwa sasa ambao wapo kwenye kiwango cha ali ya juu kwa kuwa mwaka huu ni wa masumbwi nchini Tanzania nimeanza na nitaendelea kusapoti na kupromot mchezo wa ngumi popote nchini

akizungumza kwa niaba ya chama kilichopewa dhamana ya kusimamia mchezo huo wa mei mosi Rais wa TPBO Yassini Abdallah 'Ostadhi' amesema watanzania wana bahati sana kwa kujitokeza promota mwenye uchu wa maendeleo kwa mabondia kwana mabondia wote wame saini mkataba na kupewa posho ya kufanyia mazoezi isipokuwa bondia mmoja tu kati ya watakaocheza march 29 ni Kaseba au Mashali jibu ndio tunasubili siku hiyo nani zaidi na atakaepata nafasi ya kuchapana na Kalama

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...