RAPA mpya wa Extra Bongo Grayson Semsekwa na mnenguaji Asha Shara juzi
walifanikiwa kukonga nyoyo za mamia ya mashabiki wa muziki
wa dansi waliojitokeza katika onyesho maalum la utambulisho wa
wanamuziki hao lililofanyika katika Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es
Salaam.
Semsekwa na Sharapova walitangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita kujiunga
na Extra Bongo wakitokea bendi hasimu ya African Stars Twanga
Pepeta tayari kujiandaa na uzinduzi wa albamu mpya ya bendi hiyo
inaoitwa Mjini Mipango itakayozinduliwa Februari 22 mwaka huu katika
Ukumbi wa Dar Live Mbagala.
Mara baada ya Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki kumpandisha jukwaani
repa huyo na kuanza kuimba vipande vya rapu zake za kwenye
nyimbo za zamani kama Regina Zanzibar, Double Double, 3x3 wadau
mbalimbali walijikuta wakishindwa kutulia vitini na kuanza kumtunza hali
iliyofanya Ukumbi mzima kuchangamka kwa mayowe ya furaha.
Kwa upande wake Sharapova alionyesha umahiri mkubwa wa kunengua sambamba
na wenzake katika shoo maalumu ya kinadada ambapo licha
kutofanya nao mazoezi aliweza kuendana na staili za mtindo mpya wa bendi
hiyo 'Kimbembe'.
wanamuziki hao wanaonguna na wenzao tayari kuingia kambini wiki hii
kujiwinda na uzinduzi wa albamu ya 'Mtenda Akitendewa'
unaosuburiwa kwa hamu na mashabiki wa muziki wa dansi.
Mtenda Akitendewa ni albamu ya nne kwa bendi hiyo iliyoasisiwa kwa mara
kwanza mwaka 2003 ikiwa na waimbaji Ally Choki, Bashiri
Uhadi, Bob Kissa, Richard Maarifa, Khalidi Chokoraa, Flora Moses, rapa
Greyson Semsekwa, (solo) Bonzo Kwembe, Efraim Joshua,George Gama
(besi) Rythm na kinanda Thabit Abdul drum (ngoma) zikipigwa na Imma
Chokolate.
Albamu ya kwanza iliitwa '3x3' ambao ni wimbo uliokuwa kwenye albamu
nyimbo nyingine ni 'Regina Zanzibar', 'Tuchunge Wazazi au Fikiri
Madinda', 'Nunu Milenium' 'Walimwengu Remix' na 'Odise'.
Albamu ya pili ilitwa 'Bullet Proof' ikiwa na nyimbo kama 'Double
Double' na 'Regina Zanzibar' kabla ya kusambaratika mwaka 2004 na bendi
hiyo kuanzishwa tena mwaka 2009 na kuibuka na 'Mjini Mipango'. | |
No comments:
Post a Comment