MENEJA wa Tuzo ya Mwanamakuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Marafiki (UWF) Mariam Shamo akifafanua jambo mbele ya washindi wa tuzo hiyo wa mwaka juzi na jana pamoja na wanahabari kuhusiana na hafla
yao wanayoitarajia kuifanya siku ya Wanawake Duniani mnamo Machi 15
mwaka huu,ambayo imepangwa kufanyika ndani ya kiota kipya cha maraha na
burudani Escape One Mikocheni jijini Dar, pembeni yake ni Mdau mkubwa wa
tuzo hizo na Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake
Tanzania Margareth Chacha.
Mjumbe
wa Mradi wa Mwanamakuka (Mwanamakuka Awards) na Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Wanawake Tanzania,Bi. Margareth Chacha akisisitiza jambo mbele
ya washindi wa Mwanamakuka mwaka 2012 na 2013 alipokuwa akiongelea siku
ya wanawake Duniani tarehe 15 mwezi ujao mbele ya waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Mradi wa
Mwanamakuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Wanawake Marafiki
(Unit of Women Friends),Bi Maryam Shamo.
WASHINDI wa Tuzo ya Mwanamakuka mwaka 2012 na 2013 wakiwa pamoja wakati walipokutana na waratibu wa shindano hilo kwa ajili ya kujipanga na Siku ya Wanawake Duniani inayotarajiwa kufanyika mnamo Machi 15 mwaka huu.
WASHINDI wa Tuzo ya Mwanamakuka mwaka 2012 na 2013 wakiwa pamoja wakati walipokutana na waratibu wa shindano hilo kwa ajili ya kujipanga na Siku ya Wanawake Duniani inayotarajiwa kufanyika mnamo Machi 15 mwaka huu.
WANAWAKE
nchini wamehamasishwa kushiriki Siku ya Wanawake Duniani itakayofanyika
Machi 15, mwaka huu jijini Dar es Salaam na kujadili masuala mbalimbali
ya kumwezesha mwanamke.
“Tutakutana Siku ya Wanawake Duniani na kujadili namna bora zaidi ya kumuwezesha mwanamke kujiinua kiuchumi,” alisema.
Alisema benki yake inafadhili washindi wanawake wajasiriamali kupitia mradi huo na inafanya hivyo kwa ajili ya kumwinua mwanawake kupitia benki yao ya wanawake.
Alisema benki hiyo inataka kuona wanawake wengi wanaingia katika shughuli za kijasiriamali na pia imejipanga kutumia matawi yake nchini kupanua wigo wa zawadi ya Mwanamakuka.
Alisema mpaka sasa ni asilimia mbili tu ya wanawake wanaotumia huduma za kibenki kati ya asilimia nane ya Watanzania wote wanaotumia huduma hizo, na sasa wakati umefika kuongeza idadi ya wanawake.
“Hali hiyo ni ya kihistoria lakini kwa sasa wanawake tunashukuru hali imebadilika tunaweza kufanyakazi mbalimbali zikiwamo za biashara,”aliongeza.
Alisisitiza umuhimu wa wanawake kujiunga katika vikundi kwa ajili ya kupata mikopo kutoka katika benki yao kufanyia shughuli zao za kijasiriamali.
Naye Meneja wa mradi wa Mwanamakuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Wanawake Marafiki (UWF), Maryam Shamo, alisema Siku ya Wanawake Duniani kutakuwa na maonyesho ya kazi za kijasiriamali za wanawake na michezo mbalimbali.
“Siku hiyo washindi wa mwaka huu watapatiwa zawadi zao, na pia mshindi wa jumla wa mwaka 2012 na 2013 atapatiwa zawadi kati ya washindi kumi waliokwisha pata zawadi,'' alisema.
Alifafanua kuwa katika kusherehekea ya siku hiyo, watu wengi wamealikwa wakiwamo akinamama wajasiriamali na wanasiasa wanawake.
Kwa upande wake, mjasiriamali mkazi wa Dar es Salaam na mshindi wa nyuma wa mradi huo, Tatu Ngao, alisema alishinda Shilingi milioni sita ambazo zimemwezesha kufanya biashara yake kwa ufanisi.
“Nilishinda kupitia biashara yangu ya kutengeneza keki...nimepanuka kwa kiwango cha kuridhisha hadi sasa,” alisema.
Zawadi ya Mwanamakuka ni mradi uliobuniwa na Kituo cha Wanawake Marafiki kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wanawake kwa ufadhili wa Benki ya Wanawake Tanzania na wadau wengine.
Naye mshindi wa pili wa mwaka jana , Leila Mwambungu alisema anashukuru mradi huo umemfanya apanuke kiakili katika ujasiriamali pamoja na kuweza kuwasaidia wanawake wenzake na kiu yake kubwa kuzidi kusonge mbele ili kuwa mfano kwa wengine.
"Nashukuru waandaji wa tuzo hii, shukrani zangu za pekee ziende kwa Mariam Shamo, Mama Margareth Chacha kwa namna wanavyowasaidia wanawake wenzao, najisikia furaha na fahari kuwa Mwanamakuka namba mbili wa mwaka 2013 na kiu yangu nifike mbali zaidi baada ya kuwezeshwa na mradi huu," alisema Leila.
No comments:
Post a Comment