Haruna Niyonzima akiwajibika uwanjani |
Wanaume kazini leo uwanja wa Taifa |
MABINGWA
wa soka nchini, Yanga wameendelea kunyanyasa timu za Comoro baada ya
leoi kuwanyuka Komorozine kwa mabao 7-0, huku winga Mrisho Ngassa
akiondoka na mpira kwa kufunga hat trick.
Yanga
ilipata ushindi huo katika mechi ya mkondo wa kwanza wa Ligi ya
Mabingwa Afrika katika pambano lililochezwa uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Yanga ilienda mapumziko ikiwa
mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 13 na beki Nadir Haroub
'Cannavaro' dakika ya 20.
Ngassa alifunga bao lake kwa kichwa
akiunganisha krosi ya Mbuyu Twite, huku bao la Haroub pia likifungwa kwa kichwa
kutokana na krosi ya David Luhende.
Kipindi
cha pili Yanga walibadilika na kuongeza kasi kwa kuwashambulia
wapinzani wao walioonekana wachovu na kupata mabao ya haraka haraka.
Didier
Kavumbagu alifunga bao la tatu dakika ya 57 kabla ya Hamisi Kiiza kufunga la nne dakika ya 59.
Ngassa
aliongeza mengine mawili na kumfanya afikishe mabao matatu (hat-trick)
dakika ya 64 na 68, huku bao la mwisho la Yanga likifungwa tena na
Didier Kavumbagu dakika ya 80.
Wacomoro hawakufanya mashambulizi ya
nguvu, hivyo kumfanya kipa Juma Kaseja wa Yanga kutokuwa na kazi kubwa.
Matokeo ya mchezo huo yamedhihirisha
ubabe wa Yanga kwa timu za Comoro, ambayo haina historia nzuri katika soka
kimataifa.
Komorozine inakuwa timu ya tatu
kukutana na Yanga kwenye michuano ya Afrika baada ya AJSM na Etoile d'Or
Mirontsy.
Januari 27, mwaka 2007 katika Ligi
ya Mabingwa Afrika, raundi ya awali Yanga iliifunga AJSM mabao 5-1 Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam na moja kwa moja kufuzu Raundi ya Kwanza, kwa sababu
hakukuwa na mchezo wa marudiano kwa kuwa Comoro hawakuwa na Uwanja wenye
kukidhi sifa za michuano ya Afrika.
Mwaka 2009, waliitoa timu
nyingine ya Comoro, Etoile de Mironsty kwa jumla ya mabao 14-1, ikianza kushinda
8-1 Januari 31 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kwenda kushinda 6-0
ugenini, wakati huo ikiwa chini ya kocha Mserbia, Dusan Kondic.
Hata hivyo mbio za Yanga ziliisha baada
ya kutolewa na mabingwa wa kihistoria Afrika, Al Ahly ya Misri kwa jumla ya
mabao 4-0, ikianza kufungwa 3-0 Machi 15 mjini Cairo na baadaye 1-0 wiki mbili baadaye Dar es
Salaam.
Kutokana na matokeo hao Yanga sasa
wanahitaji ushindi wowote, sare ama wasifungwe zaidi ya mabao 7-0 ili waingie
raundi inayofuata, ambapo watacheza na Ahly , ambao ndio mabingwa watetezi wa
Afrika.
Yanga: Juma Kaseja, Mbuyu
Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Kevin Yondan/Rajab Zahir, Frank Domayo,
Simon Msuva/Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Hamisi Kiiza, Mrisho Ngassa na
David Luhende/Didier Kavumbangu.
No comments:
Post a Comment