Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 19, 2014

SOMA SIMULIZI HILI LA MSANII AT


Msanii Ali Ramadhan 'AT'
SIMULIZI la kusikitisha ambalo ni la kweli na tunaweza kulitaja kama ‘simulizi la kusikitisha zaidi
la uhalisia lililowahi kusimuliwa kwenye media na msanii mkubwa wa Tanzania. Hata hivyo msanii
huyo aliiambia tovuti ya Times Fm Dar es salaam, kuwa hakuwahi hata siku moja kuyaweka masimulizi haya kwenye media wala kumsimulia mtu asiye wa familia yao.
Hii ni kwa ajili yako msomaji,


''Mimi nina kitu ambacho nadhani watanzania wengi hawakijui na ni kwa sababu sijawahi kukizungumza kokote ila tu ni kwa heshima yenu na heshima ya watanzania. Mimi nimeanza kutembea nikiwa na umri wa miaka mitano.''

Tangu nilipozaliwa nilikuwa tu nipo, natambaa kama kawaida lakini baada ya miaka mitano ndio
nikaanza kutembea kwa sababu nilikuja nikaumwa mpaka hakuna aliyeweza kufikiria kama ningepona katika familia na mwili wangu ulikuwa una usaha mwili mzima. Mfano, ukichukua wembe ukichinja kwenye mwili haitoki damu inatoka usaha, kwa hiyo kitu ambacho kilikuwa kinapelekea watu wanashindwa kukaa kwa sababu ya harufu, ulikuwa unatoa harufu sana.

Mama yangu mwenyewe siku moja aliwasikia watu wanazungumza kuwa huyu mtoto hawezi kupona,
kama sio kesho basi kesho kutwa tunaenda kuzika. Kitu ambacho wamekuja kushangaa baada ya kuja kuniona mimi mzima na nakwenda. Lakini nimeanza kutembea nina miaka 5, watoto walikuwa wananishangaa jitu zima najifundisha kwenda. Wenyewe watoto wadogo wanaenda nawekwa nichezeze nao lakini siwezi nalia, inabidi watoke watu waje kunichukua.

Yaani hakuna mtu hata mmoja anaamini kwamba yule mtoto ambaye alikuwa anaumwa tukawa
tunafikiria marehemu, leo hii atajulikana Tanzania nzima na atakuwa mtu maarufu na anafanya
shughuli zake anaruka na kucheza.

Na ilikuwa inafikiria kipindi, kama mvua inataka kunyesha wiki moja kabla watu wanatizama majira
kupitia mimi, miguu yangu kwanza lazima ivimbe, na ukibonyeza hivi kama umebonyeza mkate
halafu inakuja juu taratibu. Kwa hiyo watu walikuwa wakiniona niko hivyo wanajua kuwa mvua inataka kunyesha. Kwa hiyo nilikuwa kama mtoto wa ajabu ajabu.

Lakini alikuja doctor mmoja mpaka leo yu hai anaitwa ‘Makwetu’ ndio aliweza kunitibia,
tungekuwa tuna imani kama hizi za sasa hivi tunazungumzia za kishirikina basi mimi ningeweza
kufa. Nilichanwa kwenye mguu kwenye miguu mpaka leo niko na kovu, nikatiwa vyuma, ikapanuliwa mifupa ya miguu, ulitoka usaa naambiwa unaweza kufika hata ndoo, yaani mwili mzima mpaka mikononi nikawa natiwa mautambi….mpaka watu wanaulizana kulikoni, karogwa au vipi. Lakini mwenyezi Mungu ndio ana
mipango yake, hakuna mtu anaweza kujua.

Kwa hiyo iliwapa ugumu sana wazazi wangu, lakini baba yangu kipindi hicho alikuwa nje (Ugiriki), na
alikuwa amekata tamaa kabisa, anajua huyu mtoto ni marehemu.

AT anaamini kutokana na simulizi la maisha yake, Mungu alikuwa amemuandaa kuwa mshindi tangu
mapema. Huyu ndiye AT, mshindi wa tuzo ya Kili aliyejizolea mashabiki wengi kwa wimbo wake
‘Nipigie’ akiwa na Stara Thomas.


Times Fm Dar es salaam

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...