MTOTO
wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga marehemu Dr Wiliam Mgimwa Bw
Godfrey Mgimwa achukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la kalenga kwa
shamla shamla kubwa katika mji wa Iringa.
Pamoja
na kuchukua fomu hiyo kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la kalenga
pia aliponda mbinu zinazotumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), katika kampeni zake na kuwa kwa upande wake amejipanga
kushinda katika uchaguzi huo.
Akizungumza
na wanahabari mara baada ya kuchukua fomu za uteuzi wa kuwania nafasi
hiyo kwa msimamizi wa uchaguzi wa wilaya ya Iringa, Pudenciana Kisaka.
Kwa
mujibu wa Kisaka saa 10 jioni ya Februari 18 ndio itakuwa siku ya
mwisho ya kurejesha fomu za uteuzi kwa wagombea wote, kampeni zitaanza
Februari 19 hadi Machi 15 na uchaguzi huo mdogo wa utafanyika Machi 16.
Kabla
ya na baada ya kuchukua fomu hizo, Mgimwa aliyetokea ofisi za CCM
Iringa Vijijini zilizopo mjini Iringa, alisindikizwa na maandamano
makubwa ya wana CCM yaliyozunguka katikati ya mji wa Iringa.
“Ni
chama kinachoongoza kwa matumizi mabaya ya fedha za umma; kampeni za
vijiji helkopta, kampeni za udiwani helkopta, ubunge nao helkopta,
kwanini wanatumia vibaya fedha wanazopata badala ya kuzitumia kusaidia
kutatua kero za wananchi?” alisema.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu aliongeza kwa kusema kwamba
sio rahisi kwa viongozi wa Chadema kuyajua matatizo ya wapiga kura
wakiwa angani.
“Ukiwa
angani unawezaje kujua kama wananchi wanahitaji mchango wa maji,
madawati, vifaa vya afya, tofali, mabati na vingine vingi, sio rahisi na
huenda wanatumia mbinu hiyo ili kukwepa kuchangia shughuli za
maendeleo,” alisema.
Alisema
CCM inayajua matatizo ya wananchi inayoendelea kuyashughulikia kupitia
Ilani yake ya uchaguzi na michango yao na wadau wengine wa maendeleo.
“Hatuhitaji
chopa katika kampeni zetu; Chadema walitumia fedha nyingi kwenye
kampeni zao za chaguzi ndogo za udiwani lakini matokeo yake wameyaona na
yamedhihirisha chopa sio suluhu ya matatizo ya watu,” alisema.
Akizungumzia
vipaumbele vyake, Mgimwa alisema muda uliobaki kabla ya Uchaguzi Mkuu
wa 2015 sio mkubwa lakini endepo atapewa ridhaa na wananchi wa jimbo
hilo kuwa mbunge wao anavyo vipaumbele alivyojiwekea.
“Zipo
baadhi ya ahadi zilizotolewa na Dk William Mgimwa ambazo
hazikutekelezwa, hizo sitazizungumzia katika kampeni zangu nikiamini
zitatekelezeka kupitia vipaumbele nilivyojiwekea endapo wananchi wa
Kalenga watanipa ridhaa,” alisema.
Alivitaja vipaumbele vyake kuwa ni pamoja na kuboresha huduma ya elimu, afya, maji, elimu, miundombinu na mawasiliano.
Katika
kuyashughulikia hayo yote nina imani yale yaliyoahidiwa na aliyekuwa
mbunge wa jimbo hilo Dk Mgimwa yatakuwa yanatekelezwa.
Huku
akikataa kuweka hadharani mipango mikakati itakayotumiwa kwenye kampeni
zake, alisema ana matarajio makubwa ya kushinda katika uchaguzi huo
kwakuwa CCM inakubalika na watanzania walio wengi tofauti na
inavyofikirika na vyama vya upinzani.
|
No comments:
Post a Comment