Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 24, 2014

BENDI YA EXTRA BONGO YAFANYA MAKAMUZI MAKUBWA DAR LIVE

BENDI ya muziki wa dansi Extra Bongo Next Level wa zee wa Kimbembe juzi ilifanikiwa kukonga nyoyo za mamia ya mashabiki wa muziki wa dansi waliohudhuria uzinduzi waalbamu mpya ya bendi hiyo ya Mtenda Akitendewa uliofanyika kaika ukumbi wa DAR LIVE MBAGALA jijini Dar es Salaam. Kivutio kikubwa katika onyesho lilikuwa ni Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki alipoingia ukumbini na gari la wagomnjwa Ambulance na kupanda jukwaani moja kwa moja kuanza kulishambulia jukwaa kwa wimbo uliobeba jina la albamu Mtenda Akitendewa.Aidha mashabiki na wadau wa muziki wa dansi walionyesa kukunwa na ubora wa sauti za waimbaji wa bendi hiyo wakiongozwa na Choki, Banza Stone,Athanas Muntanabe na Richard Maarifa na Adam Bombole.Safu ya unenguaji ya bendi hiyo ikiongozwa na Super Nyamwela, Otilia Boniface ililishambulia jukwaa kwa shoo mpya ya Kimbembe na kuwafanya mashabiki wengi walihudhuria onyresho hilo kushindwa kutulia vitini hali iliyoleta msisimko mkubwa ukumbini hapo.Katika onyesho hilo Extra ilisindikizwa na bendi ya Mashujaa ambayo nayoilifanya mambo sawasawa, huku pia malkia wa mipasho Khadija Kopa akinogesha uzinduzi huo. Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Lina Sanga na Amin nao walikuwa sehemu ya burudani muhimu zilizopamba ukumbini hapo na kufanya onyesho kuacha midomo wazi wadau wa muziki waliofurika ukumbini hapo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...