Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 24, 2014

WAMILIKI WA MAENEO YA BIASHARA WAOMBWA KUTOA KIPAUMBELE KWA WANAWAKE WAJASIRIMALI



DSC_0935
Mwenyekiti wa Tancraft, Elihaika Mrema akizungumza na waandishi wa habari umuhimu wa jumuiya kubwa za wafanyabiashara na pamoja na serikali kuwaunga mkono wajasirimali wanawake nchini, Kushoto ni Esther Kasenga Msaidizi wa Katibu, Kulia Mweka hazina wa Chama cha Tancraft, Bi.Louise Judicate na Wapili kulia ni Katibu wa Tancraft, Bi. Vicky Shayo.
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania

WAMILIKI Wote wa maeneo ya biashara nchini wameombwa kutoa nafasi ya maeneo ya biashara kwa wajasirimali wanawake ili kumkomboa mwanamke kutoka katika dimbwi la umaskini na utegemezi. MOblog inaripoti. Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wajasirimali wanawake jijini Dar es Salaam leo mchana, Mwenyekiti wa Tanzania Handcraft Association (Tancraft), Elihaika Mrema amesema kuwa wanawake wafanyabiashara wadogo wana matatizo na changamoto kadhaa mojawapo ni maeneo ya kuuzia bidhaa zao.
DSC_0939
Pichani juu na chini ni Baadhi ya Wajasiriamali Wanawake wakifuatilia hotuba ya mwenyekiti wa TANCRAFT Bi. Elihaika Mrema alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la Biashara la DAR FREE MARKET lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Kenya nchini.
“hata kama mjasirimali mwanamke ukimpa mtaji wa biashara na mafunzo changamoto kubwa ni kupata eneo la kuweza kuuza hiyo bidhaa yake aliyotengeneza kwa mikono yake mwenyewe,” amesema Mrema
Mwenyekiti, Mrema amesema kuwa chama cha Tancraft kilianzishwa mwaka 2006 chini ya usimamizi wa Board of External Trade (BET) na Small industrial Development Organization (SIDO) na kina wanachama zaidi ya 300 kutoka mikoa yote Tanzania.
DSC_0937
DSC_0967
Hii ni moja ya zawadi ya kikombe kwa Chama cha Wajasiriamali Wanawake Tanzania (TANCFRAFT) walichowahi kupata kwa kuonyesha bidhaa zenye ubora wa kimataifa.
Amesema kuwa Tancraft ni chama cha wajasirimali wanaotengeneza bidhaa kwa kutumia mali ghafi za kutoka nchini kama vile nguo za batik, vikapu, minyaa, vitu vya ufinyanzi,vinyago, shanga, bidhaa za ngozi, chakula na usindikaji wa aiana zote zikiwemo asali.
“malengo makuu ya chama yalikuwa ni pamoja na kuwatafutia wanachama wake soko la pamoja kwa ajili ya kuuzia bidhaa zao,” alilisisitiza Mrema
Amesema kwamba chama cha wanawake wa wajasirimali kimepata sehemu ya Dar es Salaam Free Market ambapo wajasirimali wakinamama watapata fursa ya kufanya biashara zao bila kulipa ushuru kama walivyokuwa katika maeneo ya Chang’ombe mikono.
DSC_0849
Mkurugenzi Mtendaji wa J & L Enterprises, Bi. Louise Judicate Mushi, akitoa maelezo ya bidhaa zake za mchai chai za aina mbili black na green tea na mishumaa, amesema kwamba Green Tea ni mchai chai wa kijani kabisa ambao umesagwa kwa matumizi bora kwa afya ya binadamu
Amesema uzuri wa kinywaji hicho unaweza kunywa kikiwa cha moto au baridi, mchai chai ni dawa ya kushusha sukari, homa, presha, misuli na sumu za mwilini.
DSC_0859
Mkurugenzi Mtendaji wa J & L Enterprises, Bi. Louise Judicate Mushi akimuonjesha aina ya chai mmoja wa waandishi wa habari kutoka kituo cha Channel Ten Bw. Salum Mkambala.
DSC_0874
Mjasiriamali Fatuma Amour kutoka kampuni ya Famour Designer, akizungumzia ubunifu wake wa mavazi na ujasirimali utengenezaji wa nguo za wakinamama na wakinababa na Carpet za ngozi, viatu vya ngozi, vikapu na Batiki. Fatuma amesema alianza biashara miaka karibu 12 iliyopita katika biashara yake ya vitu vya asili vya kiafrika na changamoto kubwa kwake ni kujitangaza. Kushoto ni mwandishi wa habari kutoka Mwananchi Communications, Bi. Maimuna Kubegeya.
DSC_0871
Maimuna Kubegeya akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na Mjasiriamali Fatuma Amour kwenye jengo la Biashara la DAR FREE MARKET lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Kenya nchini ambapo watakuwa hapo kwa muda wa mwaka mmoja.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...