KAMPUNI mpya ya usambazaji wa filamu Bongo ya Yuneda
Entertainment imeingia katika biashara ya usambazaji baada ya kilio cha wasanii
kukosa sehemu za kuuza filamu zao au kusambaziwa, kampuni hiyo inayojali ubora
kwa kazi za sinema imeingia nchini kuanza kwa kusambaza filamu ya Why Linah?
Filamu hiyo iliyoshirikisha wasanii nyota katika
tasnia ya filamu Bongo kama Hemed Suleiman ‘Phd’, Rose Ndauka, Charles Magali
‘Mzee Magali’, pamoja na wasanii wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu
Swahilihood, filamu hiyo inaingia leo jumatatu.
Wasanii wamefurahia sana ujio wa kampuni hiyo kwani
wanaamini kuwa wengi wataweza kusambaziwa kazi zao kwani moja ya sifa hiyo ni
ya kizalendo inayojali maslahi ya wasanii, na inaongozwa na wazalendo wanaojua
hali halisi ya soko la filamu nchi Tanzania.
Hivyo kwa kuzingatia umakini na ubora wa filamu Yuneda
Entertainment wanakuletea filamu yenye viwango vya kimataifa ya Why Linah?.
No comments:
Post a Comment