Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, February 20, 2014

WARSHA YA KWANZA YA WADAU WA MFUKO WA MISITU TANZANIA INAYOFANYIKA MKOANI MOROGORO



Bango linalo onesha warsha ya kwanza ya Wadau wa Mfuko wa Misitu Tanzania

 Wadau mbalimbali wa Misitu wakiwa katika warsha hiyo mjini Morogoro 

****************************
Mfuko wa Misitu Tanzania ni Mfuko wa hifadhi ambao umeanzishwa kisheria kama njia endelevu ya kuwezesha uhifadhi wa rasilimali za misitu hapa nchini.Mfuko huu umeanzishwa kwa lengo la kukabiliana na changamoto za usimamizi wa rasilimali za misitu hasa katika kuimarisha utekelezaji wa Sera na Sheria ya Misitu.



Mfuko ilianza kazi rasmi Julai 2011.Mfuko wa Misitu Tanzania ni wa Umma na unasimamiwa na Bodi ya Wadhamini.Katika utendaji wa kila siku,Bodi ya Wadhamini inasaidiwa na Sekretarieti.
Mfuko wa Misitu Tanzania unafanya shughuli zake maeneo yote ya Tanzania Bara ambapo hutoa ruzuku kwa wadau wote wanojihusisha na usimamizi wa rasilimali za misitu na uboreshaji wa hali ya maisha ya wananchi waishio pembezoni wa misitu
Wadau wa Mfuko
Wadau wa Mfuko wa Misitu Tanzania ni kama ilivyoanishwa katia muongozo wa uendeshaji Mfuko ni pamoja na jamii;Asasi za jamii;watafiti na Taasisi za Utafiti; wanamazingira;Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania;Tasisi za mafunzo ya misitu na nyuki;Wizara ya Maliasili na Utalii;Serikali za Mitaa zikiwemo Halimashauli za Wilaya;Taasisi zisizo za kiserikali ( NGOs) na Asasi za kiraia.
Dhumuni la warsha hii  lilikuwani kujadiliana na wadau kuhusiana na mambo ya fuatayo
Dira
Kuwa chanzo cha muda mrefu na endelevu cha fedha za kughalamia usimamizi wa rasilimali misitu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Dhamira
Mfuko unahakikisha upatikanaji endelevu wa fedha za kugharamia usimamizi wa rasilimali misitu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Pia kuelewesha wadau na kujudiliana nao dhumuni na majukumu ya Mfuko kama ifutavyo:
Madhumuni ya Mfuko kama yalioanishwa katika kifungu cha 80 cha Misitu Sura ya 323 ya mwaka 2002.
Majukumu ya Mfuko
(i) kuhamasisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko.
(ii) kutoa ruzuku kwa wadau wa misitu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya uhifadhi na uendelezaji wa misitu katika maeneo ya usimamizi yaliopo nje ya maeneo ya wakala wa Huduma za Misitu Tanzana.
(iii) Kutangaza Mfuko kwa lengo la kupata wafadhili.
(iv) Kuhakikisha shughuli za Mfuko na miradi iliyofadhiliwa na Mfuko inatekelezwa kulingana na kanuni na miongozo.
(v) Kujenga uwezo wa watendaji wa Mfuko juu ya usimamizi wa rasilimali za misitu na za Mfuko
Warsha pia inajadili jinsi gani ya kuutangaza Mfuko ndani na nje ya nchi kwa kushirikiana na Wadau wa Mfuko
Changamoto zinazokabili Mfuko wa Misitu Tanzania.
Kuwezesha miradi zaidi a 200 kwa kipindi cha miaka mitatu bado Mfuko unakabiliwa na uhaba wa fedha kulingana na matarajio a wadau.Kwa sasa chanzo cha mapato ya Mfuko ni serikali kutoka kwenye vyanzo vilivyoainishwa kwenye sheria ya misitu ya mwaka 2002 .Hivyo mikakati ya muda mfupi na a muda mrefu inahitajia kwa ajili ya kutafuta vyanzo zaidi vya mapato nje ya serikali.Mfuko wa misitu Tanzania umeanza mchakato wa kuandaa mkakati wa kutafuta vyanzo zaidi vya fedha ili kuboresha mapato yake
Wadau watajadili Changamoto zinazokabili Mfuko wa Misitu Tanzania na nini kifanyike kupunguza changamoto hizo kama si kuziondoa kabisa ,Sekretarieti wakiwa katika mikakati ya kuhakikisha mkutano huu unakwenda sawasawa


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...