Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza kudhamini tuzo za
Mwanamakuka zenye lengo la kusaidia wanawake kutoka katika maeneo
mbalimbali kujiinua kiuchumi
Tuzo
za Mwanamakuka zinaandaliwa na The Unity of Women friends kila mwaka
zikiwatambua wanawake jasiri waliopambana kubadili maisha yao kutoka
katika hali ngumu, duni na umaskini
Akiongea
kuhusu udhamini wa Tuzo hizo Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde
alisema” Airtel inaamini kwamba ujasiriamali ni muhimu katika kufikia
maendeleo ya kiuchumi na kuondoa umaskini. Kwa kudhamini tuzo hizi za
mwanamakuka tunajikita katika kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi
na kuwa sehemu ya shughuli za maendeleo ya wanawake nchini”.
Kwa
miaka mitatu mfululizo Airtel tumekuwa moja ya wadhamini wa tuzo hizi
za mwanamakuka ambazo zimebadili maisha ya wanawake na kuwawezesha kuwa
wafanyabiashara wenye mafanikio. Tutaendelea kuonyesha dhamira yetu
katika mipango ambayo itasaidia wanawake walio katika mazingira magumu
kujikwamua kiuchumi na kukuza maendeleo ya taifa."
Jane
aliongeza kwa kusema , kuna msemo unaosema ukimwezesha mwanamke
umewezesha jamii nzima. Airtel tumejipanga kuwawezesha wanawake kiuchumi
kwani tunaamini kwa kufanya hivyo tutakuwa tumewezesha jamii kwa ujumla
Kwa upande wake mwenyekiti na Mratibu wa Mradi wa The
Unity of Women friends Maryam Shamo alisema” Tunashukuru Airtel kwa
kushirikiana nasi katika kufanikisha tuzo hizi ambazo ushirika huu
umekua wa mafanikio makubwa. Lengo la tuzo hizi ni kuwahamasisha na
kuwavutia wanawake kufikia ndoto zao. Lakini hasa tuna hakikisha kuwa
zoezi hili na matokeo yake yanaleta mafanikio ya kudumu na kubadili
maisha yao”
Tuzo
za mwanamakuka za mwaka huu zitafanyika sambamba na kusherehekea siku
ya wanawake Dunia, Mwanamakuka family bonanza itafanyika tarehe 15 machi
2014 , siku ya Jumamosi katika viwanja vya Escape 1 Dar es Saalam
kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 2 Usiku.
No comments:
Post a Comment