JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA
MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
UZIMAJI MITAMBO YA MFUMO WA UTANGAZAJI WA ANALOJIA AWAMU YA
PILI
1.0 UTANGULIZI
Mamlakaya
Mawasiliano imepokea matokeo ya tathmini ya zoezi la uhamaji toka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda kidijitAali.
Zoezi hili lilifanyika kwenye miji saba kama ilivyotajwa kwenye taarifa iliyotolewa na wataalamu wa
Chuo kikuu cha Dar e salaam waliofanya tathmini ya Uzimaji wa Mitambo ya Analojia katika Awamu ya
Kwanza.
Mamlakaya
Mawasiliano
Tanzania (TCRA) ilifanya kamisheni kwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam
kufanya tathmini ya uzimaji wa Mitambo ya Analojia katika Awamu ya
Kwanza, ikitambua kuwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kuna wataalamu wenye
uzoefu mkubwa wa kufanya tathmini za aina mbalimbali, na kwamba uzoefu
huo utasaidia sana kuhakikisha kuwa tunapata taarifa ya uhakika
itakayotuwezesha kuboresha zoezi hili kwenye awamu inayofuata.
Nachukua
nafasi hii kuwapongeza wataalamu waliohusika katika tathmini hii kwa
weledi wao kwenye kazi hii muhimu kwa taifa letu kulingana na matokeo
yaliyowasilishwa kitaalamu mbele yenu waandishi wahabari leo hii.
Tanzania
ninchiya
kwanza kuzima mitambo ya analojia Barani Afrika. Uamuzi wa kufanya
hivyo,
na matokeo yake, umeiletea sifa kubwa nchi yetu kwa jinsi ambavyo
Tanzania ilijipanga na kutekeleza maazimio yaliyofikiwa kimataifa
kwa wakati na weledi mkubwa.
Hii
imeonyesha wazi jinsi Serikali ilivyo weza kushirikiana na taasisi zake
pamoja na wadau wote katika kutimiza azma hii iliyoafikiwa kimataifa
tangu
2006.
Zoezi
la uzimaji mitambo kwa awamu ya kwanza iliyoanza taree 31 disemba 2013 haikuwa rahisi kama wengi wetu tunavyoweza kufikiria,
kwani liligusa nyanja nyingi zikiwemo za kijamii, kibiashara, kiufundi na Kisiasa.
Mamlaka
kama mdhibiti wa sekta ya Mawasiliano, ilibidi kuzingatia matakwa ya
nyanja zote na wadau mbalimbali bila kuathiri utoaji wa habari nchini.
Inakadiriwa kuwa mpaka kumaliza zoezi hili, mitambo ya kurushia matangazo kwa mfumo wa analojia isiyopungua
60 itakuwa imezimwa.
Hali hii imefanya Tanzania kuwa nchi ya pekee na kuifanya nchi yetu kuwa kituo
cha mafunzo kwa nchi nyingi ambazo sasa zimeku wazi kufika kujifunza hapa nchini.
Uamuzi wa kufanya mkutano wa nchiza SADC na ule
wa nchi za Jumuiya ya Madola kuhusu Mfumo mpya wa utangazaji wa kidijitali kwa sekta
ya utangazaji hapa nchini hivi karibuni, matokeo ya mafanikio makubwa tuliyoyapata
kwenye zoezi hili lililoendeshwa kitaalamu na Serekali yetu kupitia Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA).
1.0
UPELEKAJI WA MKONGO WA
TAIFA KWENYE VITUO VYA KURUSHIA MATANGAZO.
Mamlaka ya Mawasiliano kwa kushirikiana na Wizara
na Kampuni ya Simu ya TTCL tuko kwenye mchakato wa kuhakikisha kuwa vituo vyote
vya kurushia matangazo vinafikiwa na mkongo waTaifa (Optic fiber cable).
No comments:
Post a Comment