Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, March 25, 2011

MASHABIKI WA MSONDO WAFURAHIA BURUDANI TOKA KWA BENDI HIYO


Baadhi ya mashabiki wa bendi ya msondo ngoma wakipiga makofi kumshangiria mwanamziki mpya wa bendi hisho Shabani Dede 'Super Motisha' baada ya kuanza kuimba katika ukumbi wa Max bar Ilala Bungoni

Rapa wa bendi ya Msondo Roman Mng'ande 'Romario' akienda sambamba na mashabiki wa bendi hiyo waliofulika kuja kumuangalia mwanamziki mpya Shabani DEde 'Super Motisha' wakati wa onesho lao lililofanyika Ilala Mwishoni mwa wiki

Thursday, March 24, 2011

KAMPUNI YA SIMU YA ZANTEL YAPUNGUZA GHARAMA


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zantel wametambulisha viwango vipya vya kupiga simu vijulikanavyo kama ‘Umoja Tariff’ kuthibitisha viwango vyake ni bora na vya gharama nafuu sokoni. Viwango vya Umoja vinamwezesha mteja wa Zantel kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa TSH 2.50 kwa sekunde ikilinganishwa na TSH 3 kwa sekunde ya mitandao mingine. Pia wateja wa Zantel watafaidika zaidi na viwango hivi vya Umoja kwa kupiga simu kwa robo shilingi (TSH 0.25) Zantel kwenda Zantel kila siku kuanzia saa 5 usiku hadi saa 2 asubuhi.

Kaimu Meneja Masoko wa Zantel Bw.Brian Karokola,akizungumza na waandishi wa habari, alisema viwango hivi vipya alisema “Zantel inaheshimika kwa ubunifu na viwango na huduma zake zinazotumikia kila sehemu ya soko. Tunafahamu kuwa wateja wetu wanapendelea nini na kupitia viwango vya Umoja tumewapa wanachotaka ambacho ni thamani inayowawezesha kuongea kwa muda mrefu kwa gharama ndogo.” Viwango vya Umoja ni kwa wateja wa Dar es Salaam na Zanzibar pekee.

Wiki iliyopita Zantel walizinduwa viwango vipya vijulikanavyo kama Twanga Zaidi kwa wateja wake wa mikoani vinavyowawezesha wateja kupiga simu kwa robo shilingi Zantel kwenda Zantel masaa 24 na TSH 1.99 kwa sekunde kwenda mitandao mingine.

“Mtandao wa Zantel unajali wateja wake na kupitia viwango vyetu vipya tunakidhi mahitaji yao ambayo ni kuwawezesha kuwasiliana muda wowote kwa gharama nafuu na bila masharti.” Alimalizia Bw. Karokola.

TIMU YA NGUMI MKOA WA ILALA YAENDELEA NA MAZOEZI

Mabondia wa Mkoa wa Ilala wakioneshana ufundi wa kutupa makonde wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika Dar es salaam juzi kushoto ni Ibrahimu Clasic na Yohana Robart
Mabondia wa Mkoa wa Ilala wakioneshana ufundi wa kutupa makonde wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika Dar es salaam juzi kushoto ni Ibrahimu Clasic na Yohana Robart

Tuesday, March 22, 2011

TUZO ZA MUZIKI ZA KILI KUFANYIKA JUMAMOSI


Maandalizi kwa ajili ya onyesho la Tuzo za Muziki za Kili yamekamilika ambapo waandaaji wa Tuzo hizo, Kampuni ya Bia Tanzania TBL, kupitia kinywaji chake cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager wametangaza wasanii watakaotoa burudani katika onyesho la utoaji wa Tuzo hizo litakalofanyika Jumamosi ya Tarehe 26, Machi 2011 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni.

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL, David Minja aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana ya kuwa Utoaji wa Tuzo za mwaka huu utapambwa na burudani tofauti kutoka kwa wasanii mbalimbali na kuogezea kuwa mwaka huu onyesho litakuwa katika mwonekano wa kisasa zaidi kulinganisha na miaka ya nyuma.

“Tumekuwa tukidhamini Tuzo hizi kwa miaka kadhaa sasa na kila mwaka tumekuwa tukionyesha staili tofauti katika uboreshaji wa Tuzo hizi. Mwaka huu tumeziboresha zaidi na nina uhakika wale watakaofika kushuhudia onyesho hili watakuwa mashahidi,” Alisema Minja

Minja alisema kuwa wasanii wanaowania tuzo hizo na wale watakaotoa burudani watakaribishwa katika ukumbi huo kwa njia ya kipekee, na kuhojiwa na vyombo vya habari. “Tumeamua kutumia wasanii wa ndani na tuna imani na wanachokifanya katika suala zima la kutoa burudani,” Alisema Minja.

Alisema lengo la Tuzo hizi zinazodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ni kufikisha muziki wa Tanzania katika kilele cha mafanikio, na kuongezea kuwa mwaka huu wameona ni vyema kuwapa nafasi kubwa wasanii wa hapa nyumbani kutoa burudani kama sehemu ya kuwapa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao katika sanaa ya muziki,” alisema Minja.

Wasanii watakaotumbuiza katika utoaji wa Tuzo hizo ni Ali Kiba, THT, Banana Zoro, Linah, Diamond, Joe Makini, C Pwaa, 20%, Mzee Yusuf pamoja na Mapacha Watatu na Stara Thomas. Halikadhalika kutakuwa na burudani ya pamoja kutoka kwa washindi wa Tuzo za Kili kwa mwaka jana.

Kwa mujibu wa Minja, Tiketi kwa ajili ya onyesho hilo zimeshaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa bei ya 25,000/- kwa tiketi za VIP na 15,000/- kwa tiketi za kawaida.

Minja alisema kuwa watu watakaolipa kiingio cha VIP watapata bia za Kilimanjaro Premium Lager bure, wakati kutakuwa na bia mia moja za Kilimanjaro Premium Lager kwa watu mia moja wa kwanza kuingia ukumbini.

Tuzo zinazoshindaniwa kwa mwaka 2010/ 2011 ni Msanii wa kike bora wa Muziki, Msanii wa Kiume Bora wa Muziki, Mwibaji bora wa Kike, Mwimbaji Bora wa Kiume, Wimbo Bora wa Taarab, Wimbo bora wa Mwaka.
Nyingine ni Wimbo bora wa Kiswahili (bendi), Wimbo bora R&B, Wimbo bora wa Hip Hop, Wimbo bora wa Ragga, Rapa bora wa Mwaka (Bendi), Msanii bora wa Hip Hop, Wimbo bora wa Africa Mashariki, Mtayarishaji bora wa Muziki, Video bora ya muziki ya Mwaka na Msanii mpya anayechipukia, Wimbo bora wa Kushirikishwa/ Kushirikisha, Wimbo bora wa asili na Wimbo bora wa Rhumba.

PATA NAKALA YAKO YA DAR LEO UPATE HABARI ZAIDI JUU YA FIFO VYA WANAMZIKI WA FIVE STARS

GAZETI LA DAR LEO LIKIWA NA MUONEKANO UPANDE WA MBELE DATE 22/3/2011 JUMANNE

airtel Hands over books to four Dar Schools

Mr Akya Ambokile, a teacher from Barabara ya Mwinyi Secondary School (left) receiving books from Beatrice Singano, Airtel Tanzania’s Head of Corporate Communications. Airtel Tanzania today handed over books worth over Tshs 4 Million Shillings as aid to four Dar es Salaam based secondary schools, as part of the company’s corporate social responsibility.
Beatrice Singano (left), Airtel Tanzania’s Head of Corporate Communications, handling over books to teaching staffs representatives of Yusuf Makamba Secondary School. Airtel Tanzania today handed over books worth over Tshs 4 Million Shillings as aid to four Dar es Salaam based secondary schools, as part of the company’s corporate social responsibility.


Airtel Tanzania, the mostly available and affordable mobile service provider in the country, today handed over books worth over Tshs four Million as aid to Dar es Salaam based secondary schools, as part of the company’s corporate social responsibility.

The benefiting schools are Barabara ya Mwinyi and Aboud Jumbe secondary schools in Temeke district and Yusufu Makamba and Turiani secondary schools in Kinondoni district.

Speaking during the books handover event at Airtel Head offices in Dar es Salaam, the company’s Corporate Social Responsibility Manager, Tunu Kavishe, said the four schools are amongst 104 schools across the country that will benefit from the unique airtel books project, following a random draw that was held early this year, involving 520 secondary schools.

“We are giving an equal opportunity to schools from all regions in the country to ensure that the books reach students from every part of the country. We have spent 104 million Shillings on buying these books so as to enable each school to get books worth one million Tanzanian shillings”, said Ms. Kavishe.

She further added that each benefiting institution had a unique opportunity to choose their ideal book requirements based on their curriculum and subjects offered at the institution. This will enable Airtel to procure and handover sets of books that adequately meet the need of each school.

“We are highly committed towards supporting communities in Tanzania by improving education levels through availing the most important tools - books - to secondary schools students. Since we started our books support programme, approximately seven years ago, we have reached more than 800 secondary schools that are spread across the country”, said Ms. Kavishe.

Apart from the 104 secondary schools benefiting from books aid, Airtel Tanzania has already adopted a rural primary school in Bagamory District – Coast Region, being a pilot project. The company has completed major refurbishment of existing structures and construction of 10 new ones.

It is expected that after this year, the initiative will be extended to more schools countrywide. Airtel will work closely with the Ministry of Education to identify them and their locations.

wasanii wa five star waliopata ajali na kufariki na wale waliojeruhiwa watajwa

wasanii wa five star waliopata ajali na kufariki na wale waliojeruhiwa watajwawasanii wa five star waliopata ajali na kufariki na wale waliojeruhiwa watajwaBaadhi ya wasamalia wema waliokuwa kwenye foleni ya magari baada ya kutokea kwa ajili ya Basi ndogo la Wasanii wa Kundi la Five Stars Moden Taarab wakichunguza kwa makini iwapo kuna mtu aliyebanwa ama kusahauliwa kuokolewa ama miili wake kubakia eneo hilo baada ya basi hilo kuparamia lori lililosheheni mbao lililokuwa limeharibika njiani , katika barabara kuu ya Iringa- Morogoro , eneo la Hifadhi ya Taifa ya wanyama ya Mikumi, karibu na Kijiji cha Doma, Wilaya ya Mvomero usiku wa kuamkia leo.
Lori lililoparamiana na basi la wanamuziki wa Five Stars

wasanii wa five star waliopata ajali na kufariki na wale waliojeruhiwa watajwaMsanii wa kikundi cha Taarab cha East African Melody Bi Mwanahawa Ally ( 55) akiwa wodini katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro leo baada ya kujeruhiwa kwenye ajali ya basi dogo la wasanii wa Kundi la Five Stars Moden Taarab la Jijini Dar es Salaam. Yeye alikuwa msanii mwalikwa kwenye safari hiyo ya kikazi katika mikoa ya nyanda za juu kusini . Picha zote na habari na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro


Majina ya wanamuziki wa bendi ya Five Star Modern Taarab waliokufa katika ajali ya gari Mikumi mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo yamefahamika.

Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Morogoro Be. Ibrahim Mwamakula, marehemu hao ni Issa Kijoti, Nasoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashim, Tizo ,Omari Tall,Ngeleza Hasan,Hamisa Omari,Maimuna 'Kisosi', Haji Msaniwa na mcheza show wa kundi la Kitu Tigo Ilala

“ Hii ajali imepoteza watu 13 kati ya hao 12 wamefariki papo hapo na mmoja
amefariki akiwa anapatiwa matibabu Hospitalini.

"Ni ajali mbaya kutokea iliyohusisha magari matatu, ambapo waliokufa wote ni kutoka kwenye basi dogo la wasanii wa kikundi cha Five Stars na kusababisha majeruhu tisa kulazwa” alisema Mwamakula, akifafanua kuwa kati ya waliokufa 10 ni wanaume na watatu ni wanawake.

Amesema majeruhi tisa ambao wote ni wasanii waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Morogoro ni pamoja na Mwanahawaa Ally( 55) kutoka Kundi la East African
Melody, ambaye alikuwa ni msanii mwalikwa, Susana Benedict(32), Zena Mohamed
(27), Samila Rajab (22)na Mwanahawa Hamisi (36)ambao wamelazwa wodi namba
tatu.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliwataja
wasanii wengine waliolazwa katika Hospitali hiyo ni pamoja na Ally Juma
(25), Rajabu Kondo ( 25), Issa Hamis , Shaaban Hamis (41) na Msafiri Musa
(22).

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, kuwa dereva huyo aliligonga lori hiyo wakati akijaribu kulikwepa Lori jingine lililokuwa likotokea mbele yake lenye namba T 530 BHY lenye tela T 182 BKB aina ya Scania ambapo katika harakati hizo basi hilo lililigonga Lori hiyo mbele pembezoni na kusababisha magari hayo kuanguka.

Alisema kuwa baada ya kuliparamia Lori hiyo , basi hilo liliyumba na kuhama uoande wake na kujibamiza kwenye Lori lililokuwa mbele yake ambalo halikuwa na mzingo kitendo kilichofanya paa la basi hilo kukatwa wa juu ambapo watu 12 waliokuwa ndani ya basi ndogo hilo kufariki dunia papo hapo na wengine saba kujeruhiwa vibaya .

Hata hivyo alisema , majeruhiwa mmoja kati ya saba alifariki dunia wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro alipofikishwa kutoka eneo la tukio na kutambuliwa na ndugu zake kuwa ni Haji Mzaniwa ( 38), mwimbaji wa kikundi hicho.

KUNDI LA FIVE STAR LAPATA AJALI 13 WAFARIKI DUNIA


HABARI YA KUAMINIKA ILIYOTUFIKIA HIVI PUNDE TOKA MKOANI PWANI,INARIPOTI KWAMBA ,BASI LA ABIRIA AINA YA TOYOTA COASTER LILILOKUWA LIMEBEBA WANAMUZIKI WA BENDI YA TAARAB YA FIVE STAR MODEN TAARAB LIMEPATA AJALI MBAYA SANA USIKU HUU NA KUSABABISHA VIFO KWA BAADHI YA WANAMUZIKI HAO NA WENGINE KADHAA KUJERUHIWA VIBAYA SANA NA KUKIMBIZWA KATIKA HOSPITALI YA TUMBI ILIYOPO KIBAHA MKOANI PWANI.

AJALI HIYO IMETOKEA USIKU HUU KATIKATI YA MKOA WA PWANI NA MOROGORO NA CHANZO CHA AJALI HIYO BADO HAKIJAFAHAMIKA MPAKA HIVI SASA.

BENDI HIYO ILIKUWA NJIANI KURUDI JIJINI DAR KUTOKEA SONGEA MKOANI RUVUMA KWA SHUGHULI ZAKE ZA KIMUZIKI.

TUNAENDELEA KUFUATILIA KWA KINA TUKIO HILO NA TUTAENDELEA KUJULISHANA KADRI TAARIFA ZITAKAVYOKUWA ZINATUFIKIA.

Saturday, March 19, 2011

MSONDO NA SIKINDE ZILIVYO ONESHANA UMWAMBA JANA

Mpiga gita la Solo Abdul Ridhiwani 'Pangamawe wa Msondo akiwapagawisha mashabiki wakati wa mpambano wao na Sikinde jana
Mashabiki wa Sikinde wakilisakata lumba
JUma Katundu akiwa sambamba na Nacho Mpendu Mama Nzawisa
Mashabiki wa Msondo wakifuraia magitaa yalivyokuwa yakikungutwa
Hasani Moshi 'Tx Jr' kushoto na Shabani Dede 'Super Motisha'
Waimbaji wa Msondo wakilishambulia jukwaa wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana
Wanamziki wa bendi ya Sikinde wakilishambulia jukwaa kulia ni Husein Jumbe, Hassani KUnyata na Abdalah Hemba
Hassani Kunyata na Husein Jumbe wakiimba
Abdalah Hemba akimba sambamba na kucheza na mnenguaji wa bendi ya Sikinde

Thursday, March 17, 2011

JK ATINGA WIZARA YA ELIMU KUKAGUA MAENDELEO

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Elimu leo
Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Balaza la Mitiani Tanzania JOys Ndarichako walipokutana wizara ya Elimu leo

Wednesday, March 16, 2011

MSONDO WASEMA NJOO UPATE KIKOMBO TOKA LOLIONDO BAADA YA KUNYAKUWA DEDE


BENDI ya muziki wa Dansi ya Msondo Ngoma inatarajia kufanya onesho la kukata na shoka katika ukumbi wa Diamondi Jubilee Jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza wakiwa na mwanamuziki mkongwe aliyejiunga na bendi hiyo jana akitokea Sikinde Shaban Dede.

Akizungumza Dar es salaam leo, Msemaji wa Bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema onesho hilo limeandaliwa na Kampuni ya Prime Time Promotions kuzishindanisha bendi za Msondo na Sikinde kupima hali ya muziki wa bendi hizo kwa sasa.

Alisema wakiwa na mwanamuziki huyo bendi hiyo itatoa burudani ya kutosha kwa wapenzi wake kwa nyimbvo zao zote za zamani na za sasa ambapo Dede ataimbisha baadhi ya nyimbo alizoimba akiwa Msondo.

Alizitaja nyimbo atakazoimbisha mwanamuziki huyo ni Benadeta, Kimwaga, Fatuma, pamoja na Sauda ambapo pia atashirikiana na wanamuziki wa bendi hiyo kuimba nyimbo mbalimbali za bendi.

Super D alisema mwanamuziki huyo alianza rasmi mazoezi akiwa Msondo leo katika ukumbi wa Amana ambapo pia atakuwa katika maonesho mbalimbali yanayowakabili likiwemo la jumamosi katika ukumbi wa TCC Chang'ombe na Jumapili watakuwa katika ukumbi wa Max Bar Ilala.

Kwa Upande wake Dede alisema wapenzi wa bendi hiyo waje kwa wingi kuburudika na kuahidi kuimba muziki wenye radha ambayo mashabiki wa Msondo wanaitaka.

Alisema sasa ameamua kufanya kazi rasmi na Msondo lengo likiwa ni kuibadilisha mazingira katika kazi yake hiyo kwa sababu bendi hizo mbili zinafanya muziki unaoshabihiana na kwamba atamalizia maisha yake ya muziki akiwa Msondo.

Alisema kwa kuanzia ametunga wimbo mmoja ambao hajaupatia jina unaozungumzia matumizi mabaya ya madawa ya kulevya ambao bado hajaupatia jina na pia katika albamu mpya iliyokwisha andaliwa na bendi hiyo mwaka huu yenye nyimbo nne ataongeza nyimbo mbili kabla ya kuingia sokoni.

Tuesday, March 15, 2011

semina ya maafisa mauzo na usambazaji wa TBL

Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa TBL,Nicholas Broks akifafanua jambo mbele ya Maafisa mauzo na usambazaji wakati wa muendelezo wa semina ya siku mbili iliyokuwa ikifanyika katika hotel ya Kunduchi Beach,jijini Dar leo.
Mmoja wa maofisa wa TBL akitoa mchanganuo wa kazi wakati wa semina ya siku mbili ya maofisa wa TBL nchi nzima iliyomalizika mchana huu katika hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar.
Wadau wa TBL wakiwa katika semina.
picha ya pamoja huku kina mmoja akiwa na furaha

UZALENDO CONCERT LAJA

Mkurugenzi wa Global Publishers Eric Shigongo (kulia) na Mkurugenzi wa Clouds FM, Ruge Mutahaba wakibalidilishana mawazo wakati wa uzinduzi wa tamasha la Uzalendo
Mwanamuziki wa Reggae aishie Marekani, Innocent Galinoma akiongea na Media

Mwanamuziki na mshairi mahiri nchini, Mrisho Mpoto, akiongea jambo na Ruge

BREAKING NEWS DEDE ATUA MSONDO NGOMA



Aliyekuwa mwimbaji wa bendi ya Sikinde Shabani DEDE kulia katangaza leo jioni kuwa amejiunga rasmi na mahasimu wao wakubwa Msondo Ngoma Music Bandi Siku mbili kabla ya mpambano wao ambapo kesho ananza rasmi mazoezi na bendi yake mpyaa

Sunday, March 13, 2011

SUPER D BOXING COACH YAINGIA MTAANI JANA



BONDIA wa Zamani na Kocha wa Ngumi wa Klabu ya ngumi ya Ashanti, Rajabu Mhamila'Super D' ameingiza Video inayozungumzia maisha yake ya mchezo huo.Akizungumza Dar es Salaam leo, Super D alisema video hiyo ilikua sokoni kuanzia sasa ikizungumzia maisha yake tangu alipoanza kucheza mchezo huo mwaka 1984 hadi 2010 sasa.Alisema Video hiyo itaonesha mapambano mbalimbali aliyocheza na dhidi yamabondia Mbwana Matumla, Rashidi Ali na Ajibu Salumu.Alisema lengo la kuandaa video ni kutaka kutimiza malengo yake ya kuendelezamchezo wa ngumi kwa kuwapatia vijana nafasi ya kujifunza kupitia kwake.Alisema kutokana na nchi ya Tanzania kuwana vipaji vingi atashindwa kuwafikiakila mmoja wao na badala yake amewapa fursa ya kujifunza kwa kuangalia video.Alisema Video ya katika kuhaikisha hiyo DVD inafanya vizuri sokoni ameongezeavionjo vingine kutoka kwa mabondia maarufu duniani kama Mike Tyson, Michael Mo,Junior Myweather, Mohamed Ally, Man aqyao na Joe Fleizer ambapo kuanzia sasa ipo mtaani ususani makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi Dar es salaam

tigo wakabidhi nissan hard body kwa mshindi wa promosheni ya bahatika

Ofisa Viwango wa Tigo, David Zakaria akikabidhi funguo ya gari aina ya Nissan Hard Body yenye thamani ya shs milioni 56 kwa mshindi wa promosheni ya Bahatika na Tigo, hafla iliyofanyika katika viwanja vya Coco Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Ofisa Uhusiano wa Tigo Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya gari ya promosheni ya Bahatika na Tigo ambako washindi wawili walikabidhiwa magari yao aina ya Nissan Hard body yenye thamani ya shs milioni 56 kila moja jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Chidi Benz akifanya vitu vyake katika onyesho hilo.
Joe Makini akiwachengua umati wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam katika onyesho la Bahatika na Tigo katika viwanja vya Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofurika katika viwanja vya Coco Beach, Dar es Salaam kushuhudia onyesho la Bahatika na Tigo ambalo washindi walikabidhiwa magari yao ainaya Nissan Hard Body.

TAMIMU AMTWANGA ASHIRAFU KILA MMOJA ALAMBA SAKAFU KWA MAKONDE

Awadhi Tamimu akilamba sakafu
Ufundi wa kutupa mawe ukioneshwa
Tamimu akirusha ngumi kwa Ashirafu
Ashirafu akilamba sakafu
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...