Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 22, 2011

KUNDI LA FIVE STAR LAPATA AJALI 13 WAFARIKI DUNIA


HABARI YA KUAMINIKA ILIYOTUFIKIA HIVI PUNDE TOKA MKOANI PWANI,INARIPOTI KWAMBA ,BASI LA ABIRIA AINA YA TOYOTA COASTER LILILOKUWA LIMEBEBA WANAMUZIKI WA BENDI YA TAARAB YA FIVE STAR MODEN TAARAB LIMEPATA AJALI MBAYA SANA USIKU HUU NA KUSABABISHA VIFO KWA BAADHI YA WANAMUZIKI HAO NA WENGINE KADHAA KUJERUHIWA VIBAYA SANA NA KUKIMBIZWA KATIKA HOSPITALI YA TUMBI ILIYOPO KIBAHA MKOANI PWANI.

AJALI HIYO IMETOKEA USIKU HUU KATIKATI YA MKOA WA PWANI NA MOROGORO NA CHANZO CHA AJALI HIYO BADO HAKIJAFAHAMIKA MPAKA HIVI SASA.

BENDI HIYO ILIKUWA NJIANI KURUDI JIJINI DAR KUTOKEA SONGEA MKOANI RUVUMA KWA SHUGHULI ZAKE ZA KIMUZIKI.

TUNAENDELEA KUFUATILIA KWA KINA TUKIO HILO NA TUTAENDELEA KUJULISHANA KADRI TAARIFA ZITAKAVYOKUWA ZINATUFIKIA.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...