Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 8, 2011

safari lager nyama choma,mbeya carnival yaibuka kidedea kwa uchomaji nyama

Katibu Tawala wa Mbeya,Damson Nthangu (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi kwa mshindi wa Nyama Choma kwa Mkoa huo ambao ni Mbeya Carnival,Mashindano hayo yamefanyika katika viwanja vya CCM,Ilomba jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Buttallah.Katika fainali hizo baa ya Mbeya Canival iliibuka mabingwa na kujinyakulia kitita cha Shilingi 1,000,000/- ,huku 2000 Grocery ikishika nafasi ya pili nakupata kitita cha sh. 800,000/-, Night Sky Club nafasi ya tatu na kupata sh. 600,000/- huku baa ya Karembu bar ikawa ya nne kwa kupata sh. 400,000/-.Fainali za Nyama choma zinatarajia kufanyika katika mikoa mingine mitatu ambapo jijini Dar es salaam Zitafanyika tarehe 13/03/2011 katika viwanja vya Leaders club, mkoani Arusha ni tarehe 26/03/2011 kwenye kiwanja cha AICC Club kisha kumalizikia kwenye Viwanja vya Glacious Vilivyopo Shant town mkoani Kilimanjaro.ambapo wakazi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro wanaendelea kupiga kura kwa kuchagua baawanayoamini inachoma nyama bomba zaidi kwa kuandika ujumbe mfupi SAFARI kisha nafasi JINA LA BAA nafasi MKOA ULIOPO kisha unatuma kwenda nambari 15540
Mshindi wa Pili 2000 Grocery akionyesha fedha alizoshinda katika shindano la Nyama Choma mkoani Mbeya lililofanyika katika viwanja vya CCM,Ilomba jijini Mbeya mwishini mwa wiki.

SKY Night Pub ilishika nafasi ya tatu katika kinyang'anyiro hicho.
kiduku kikichukua nafasi yake mara baada ya ushindi wa kwa wana Mbeya Carnival.
furaha ya ushindi.
Mgeni Rasmi akiwasili katika viwanja vya CCM,Ilomba Jijini Mbeya.
Majaji wakipitisha vipimo vyao.
Majaji wakiandika maelezo wakati wakipitia wachoma nyama wa jijini Mbeya.
Wadau wakikata kiu na kilaji cha Safari Lager wakati wakisubiria Nyama Choma.
Wadau wakiwakilisha jijini Mbeyai.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...