Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, March 30, 2011

BENDI YA MASHUJAA KUTAMBULISHA WAPYA APRIL 1 KIJIJI CHA MAKUMBUSHO


BENDI ya Mashujaa Musica Aprili 1 mwaka huu inatarajia kufanya onyesho la utambulisho wa wanamuziki wake wapya waliojiunga na bendi hiyo wakitokea bendi mbalimbali za nchini na Kinshasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika Ukumbi wa Mgahawa wa Hadees, Meneja wa bendi hiyo, Mujibu Hamis, alisema kuwa maandalizi ya onyesho la utambulisho wa wanamuziki limekamilika kwa asilimia 99 na aslimia moja ikibaki kuwa ni onyesho lenyewe litakalofanyika katika Ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho.


Aidha alisema kuwa onyesho hilo ni maalum kwa ajili ya kutambulisha wanamuziki wapya, lakini pia ni maalum kwa ajili ya kuwapa raha mashabiki wa bendi hiyo na kuonyesha kile kilichowafanya kukaa kimya kwa kipindi wakijipanga zaidi.


“Tumejiandaa vilivyo kuwaonyesha mashabiki wa muziki wa dansi ujio mpya wa bendi yetu iliyokuwa kimya kwa ajili ya kujipanga ili kuweza kwenda na wakati katika jukwaa la ushindani la Muziki wa dansi, na pia tumejitahidi kuongeza wanamuziki katika kila idara kuanzia waimbaji hadi wanenguaji ili kuweza kutoa burudani iliyokamilika kwa mashabiki wetu” alisema Mujibu.


Aliwataja wanamuziki hao wapya wanajiunga na bendi hiyo kuwani pamoja na, Kajo anayetoka katika Kundi la Boziboziana, Jimmy Adol kutoka kwa Koffee Olomide, Profa Kariakoo kutoka Kinshasa, Kama Simba Komilion, kutoka kwa Felix Wazekwa.


Wengine ni Rapa mahiri Sauti ya Radi, Kelvin, Salma Shaban ‘Teketeke’ Mariam Lelapel na Corando wote kutoka bendi ya Diamondi Musica.


Katika onyesho hilo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa bendi inayoongozwa na vijana watatu ‘Mapacha 3’, bendi yenye umri wa mwaka mmoja tangu ilipoanzishwa na kuweza kujizolea sifa kem kem baada ya kutwaa Tuzo mbili katika Kili Music Awards 2010, ambazo ni Tuzo ya Wimbo Bora wa bendi wa 2010 pamojana Tuzo ya Rapa bora wa bendi wa mwaka 2010.

Rapa Mahiri wa bendi ya Mashujaa Musica, aliyejiunga na bendi hiyo akitokea bendi ya Diamond Musica, Yanick Noa ‘Sauti ya Radi’ (kulia) akigahan sehemu ya rap zake wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana kuhusu onyesho la utambulisho wa wanamuziki wapya waliojiunga na bendi hiyo, linalotarajia kufanyika April 1 kwenye ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho. Katikati ni Meneja wa bendi hiyo, Mujibu Hamis na Kiongozi wa bendi hiyo, Jado Fidforce pamoja na wanenguaji wa bendi hiyo. ******************************** Wanenguaji wa bendi ya Mashujaa Musica Salma Shaban ‘Teketeke’ (kulia) na mariam Ramadhan ‘Lelapee’, wakionyesha umahiri wao wa kushambulia jukwaa wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam jana, kuhusu onyesho la utambulisho wa wanamuziki wapya waliojiunga na bendi hiyo, linalotarajia kufanyika April 1 kwenye ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho
http://sufianimafoto.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...