Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 8, 2011

MAHAKAMA YAIAMBIA SEREKALI KUWA AINA HAKI YA KUVUNJA NYUMBA PASIPO MAKUBALIANO YA KIMAHAKAMA


UPANDE wa serikali katika kesi ya ardhi namba 213 ya mwaka 2010 kati ya serikali na wakazi wa kota za Gerezani wanaotakiwa kuhama eneo hilo kupisha ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo kasi umeiomba mahaka Kuu ya Ardhi kuwaruhusu kutafuta ufumbuzi wa suala hilo nje ya mahakama.

Ombi hilo limetolewa mahakamani hapo na mawakili upande wa serikali ambao hawakutaka kutaja majina yao mbele ya Jaji aliyetambulika kwa jina la Bi.A.Ngwala

Jaji ngwala alikubaliana na ombi hilo na kusema kuwa shauri hilo litapelekwa kwa jaji mfawidhi katika mahakama ya Rufaa ili kutafutiwa msuluhishi atakayesikiliza mazungumzo hayo.

Alisema kama mazungumzo hayo yatafikiwa muafaka kesi hiyo itafutwa rasmi na kama hawatakubaliana itarudishwa tena mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa.

Alisema suluisho la kesi hiyo linatakiwa kufikiwa haraka iwezekanavyo ili wananchi waweze kujua hatma yao bila ya kutoa visingizio vya mahakama kuwa inachelewesha.

Katika hatua nyingine Jaji Ngwala aliwataka mawakili wanaoiwakilisha serikali kuwatoa taarifa ya mwenendo wa kesi hiyo kwa wateja wao ili kuepuka migongano inayojitokeza.

"Ninyi wanasheria mnatakiwa kueleza wateja wenu kila kitu ili kuepuka migongano,haiwezekani kesi bado ipo mahakamani alafu masuala mengine yanaingiliwa kati,zuio lililotolewa awali la kutovunja nyumba hizo mpaka kesi itakapokwisha bado lipo palepale"alisema.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...