Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, March 16, 2011

MSONDO WASEMA NJOO UPATE KIKOMBO TOKA LOLIONDO BAADA YA KUNYAKUWA DEDE


BENDI ya muziki wa Dansi ya Msondo Ngoma inatarajia kufanya onesho la kukata na shoka katika ukumbi wa Diamondi Jubilee Jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza wakiwa na mwanamuziki mkongwe aliyejiunga na bendi hiyo jana akitokea Sikinde Shaban Dede.

Akizungumza Dar es salaam leo, Msemaji wa Bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema onesho hilo limeandaliwa na Kampuni ya Prime Time Promotions kuzishindanisha bendi za Msondo na Sikinde kupima hali ya muziki wa bendi hizo kwa sasa.

Alisema wakiwa na mwanamuziki huyo bendi hiyo itatoa burudani ya kutosha kwa wapenzi wake kwa nyimbvo zao zote za zamani na za sasa ambapo Dede ataimbisha baadhi ya nyimbo alizoimba akiwa Msondo.

Alizitaja nyimbo atakazoimbisha mwanamuziki huyo ni Benadeta, Kimwaga, Fatuma, pamoja na Sauda ambapo pia atashirikiana na wanamuziki wa bendi hiyo kuimba nyimbo mbalimbali za bendi.

Super D alisema mwanamuziki huyo alianza rasmi mazoezi akiwa Msondo leo katika ukumbi wa Amana ambapo pia atakuwa katika maonesho mbalimbali yanayowakabili likiwemo la jumamosi katika ukumbi wa TCC Chang'ombe na Jumapili watakuwa katika ukumbi wa Max Bar Ilala.

Kwa Upande wake Dede alisema wapenzi wa bendi hiyo waje kwa wingi kuburudika na kuahidi kuimba muziki wenye radha ambayo mashabiki wa Msondo wanaitaka.

Alisema sasa ameamua kufanya kazi rasmi na Msondo lengo likiwa ni kuibadilisha mazingira katika kazi yake hiyo kwa sababu bendi hizo mbili zinafanya muziki unaoshabihiana na kwamba atamalizia maisha yake ya muziki akiwa Msondo.

Alisema kwa kuanzia ametunga wimbo mmoja ambao hajaupatia jina unaozungumzia matumizi mabaya ya madawa ya kulevya ambao bado hajaupatia jina na pia katika albamu mpya iliyokwisha andaliwa na bendi hiyo mwaka huu yenye nyimbo nne ataongeza nyimbo mbili kabla ya kuingia sokoni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...