Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, March 13, 2011

SUPER D BOXING COACH YAINGIA MTAANI JANABONDIA wa Zamani na Kocha wa Ngumi wa Klabu ya ngumi ya Ashanti, Rajabu Mhamila'Super D' ameingiza Video inayozungumzia maisha yake ya mchezo huo.Akizungumza Dar es Salaam leo, Super D alisema video hiyo ilikua sokoni kuanzia sasa ikizungumzia maisha yake tangu alipoanza kucheza mchezo huo mwaka 1984 hadi 2010 sasa.Alisema Video hiyo itaonesha mapambano mbalimbali aliyocheza na dhidi yamabondia Mbwana Matumla, Rashidi Ali na Ajibu Salumu.Alisema lengo la kuandaa video ni kutaka kutimiza malengo yake ya kuendelezamchezo wa ngumi kwa kuwapatia vijana nafasi ya kujifunza kupitia kwake.Alisema kutokana na nchi ya Tanzania kuwana vipaji vingi atashindwa kuwafikiakila mmoja wao na badala yake amewapa fursa ya kujifunza kwa kuangalia video.Alisema Video ya katika kuhaikisha hiyo DVD inafanya vizuri sokoni ameongezeavionjo vingine kutoka kwa mabondia maarufu duniani kama Mike Tyson, Michael Mo,Junior Myweather, Mohamed Ally, Man aqyao na Joe Fleizer ambapo kuanzia sasa ipo mtaani ususani makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi Dar es salaam

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...