Baadhi
ya wachezaji wa timu ya Coast Union ya jijini Tanga, wakiwa katika
Bandari ya jijini Dar es Salaam jana mchana, wakati wakielekea kupanda
Boti kwenda Zanzibar kwa ajili ya kuanza kambi yao ya wiki moja
kujiandaa na Ligi Kuu ya Tanzania Bara inayotarajia kuanza Septemba 15,
mwaka huu.
Wakielekea kupanda Boti.
TIMU
ya Coast Union ya jijini Tanga imeondoka jana jijini Dar es salaam,
kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki moja kwa ajili ya
kujiandaa na Ligi Kuu ya Tanzania Bara inayotarajia kuanza Septemba 15,
mwaka huu.
Timu
hiyo iliyo chini ya walimu wake, Juma Mgunda na Habib Kondo, leo
asubuhi imeanza mazoezi yake katika Viwanja vya Shangani Mnazi Mmoja,
ikiwa na wachezaji wake wote.
Akizungumza
na mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, Kocha msaidizi wa
timu hiyo, Habib Kondo, alisema kuwa wameamua kuweka kambi mjini Unguja
ili kufanya maandalizi ya kutosha kuelekea Ligi Kuu.
Aidha
Kondo, alisema kuwa wakiwa mjini Zanzibar ili kufanikisha na kutimiza
malengo ya kambi yao timu hiyo itakishirikisha Chama cha Mpira wa Miguu
cha Zanzibar ZFA ili kuwasaidia kupata mechi za kirafiki na timu za
Visiwani humo.
''Mpaka
sasa tayari tumeshapata mechi mbili za kirafiki, ambapo kesho tutashuka
dimbani katika uwanja wa Amani, kukipiga na timu ya Falcon, na mechi
itakayofuata tutacheza na timu ya Mafunzo,
Kiukweli
tunashukuru Mungu tumejitahidi kupata timu nzuri na tumejipanga kufanya
vizuri si kushiriki Ligi Kuu tu bali kutetea nafasi nne za juu katika
Ligi ya mwaka huu, na ninaamini iwapo hakutakuwa na longo longo na
mizengwe ya kubebwabebwa kwa baadhi ya timu basi wasitegemee mtelemko
kutoka kwetu, wajiandae kupambana''. alisema Habib
Timu
hiyo inatarajia kumaliza kambi yake hiyo ya maandalizi ya Ligi Kuu,
Septemba 10, mwaka huu na kurejea jijini Tanga ambako ndiyo Maskani yake
makuu.
No comments:
Post a Comment