Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF, Prof.Ibrahim Lipumba akiwasili kwenye Mkutano wa Chama hicho uliofanyika Jangwani jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wananchi na wanachama wa chama hicho waliojitokeza kwenye mkutano huo.
Wafuasi wa Chama hicho wakifurahia jambo.
Kikundi cha Mchiriku nacho hakikua mbali kutumbuiza.
Kadi za vyama mbalimbali zilirejeshwa na kukabidhiwa kadi mpya.
Afande Sele nae alitumbuiza kwenye mkutano huo.
Msanii Kala Pina, akitoa burudani
kwa wanachama wenzake wa chama hicho, kwenye uchaguzi wa 2010, Kalapina
aligombea udiwani kupitia chama hicho kwenye kata ya Kinondoni.
KATIKA kile kinachoonekana ni kujipanga kisiasa kuelekea
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Chama cha wananchi CUF leo kimezindua mkakati mpya
wa kujiimarisha nchi nzima.
Akiwahutubia maelfu ya wanachama waliohudhuria kwenye
mkutano mkubwa Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba pamoja na mabo
mengine ya kiuchumi wa dunia na wa hapa nchini lakini hakuacha kugusia mkakati
wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015.
Alisema chama chake kimejipanga kimkakati kuelekea uchaguzi
huo na anaamini watanzania watakiunga mkono kwani ni ndio chama pekee chenye
sera mbadala za kuleta mabadiliko. Aidha Prof. Lipumba alisema uchumi wa dunia
kwasasa uko katika halimbaya sana lakini hali mbaya hiyo inatoa fursa kwa nchi
masikini kujiimarisha kupitia kilimo kutokana na bei ya mazao ya kilimo
kuongezeka duniani kote.
Aidha Lipumba alifafanua kuwa kuongezeka kwa mahitaji ya
mazao ya kilimo kunatokana pia na kuimarika kwa uchumi kwenye nchi ambazo zina
watu wengi akitoa mfano wa China na India ambazo zinawatu zaidi ya bilioni moja
.
Awali akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano
huo Naibu Mkurugenzi wa habari na uenezi wa Chama hicho Abdull Kambaya, alisema
tabia ya chadema ya kuisema CUF kama ni CCM B, ni yakuficha ukweli kwamba wao
ndio CCM B kwa kuendesha chama chao chini ya misaada ya makada wa CCM akiwamo
kada maarufu wa chama hicho Mustafa Sabodo. Hata hivyo akahoji kuwa kitendo cha
chama hicho kwenda kuombaomba CCM kupata wagombea ni kitendo cha kutojiamini.
No comments:
Post a Comment