Mwenyekiti
wa Chama cha waendesha Bodaboda Mkoa wa Rukwa Ndugu Farjala Hussein
akielezea mikakati ya kuimarisha chama chao pamoja na kuwasilisha ombi
lao kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye hayupo pichani kuwa mlezi wa chama
hicho.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na viongozi wa
chama cha waendesha pikipiki za biashara maarufu kama Bodaboda Mkoa wa
Rukwa ofsini kwake alipotembelewa na vongozi hao kujadili mambo
mbalimbali yanayohusu umoja wao ambapo walimuomba kiongozi huyo kuwa
mlezi wa chama chao ambacho kinaanza kujijenga. Kulia ni Mwenyekiti
mteule wa chama hicho ndugu Farjala Hussein. Mkuu huyo wa Mkoa alikubali
ombi lao na kuwaahidi ushirikiano kwa kuwasaidia kuboresha huduma zao
kwa wananchi wa Mkoa wake wa Rukwa.
Kikao
hicho kilichumuisha pia maafisa ushirika kutoka Manispaa ya Sumbawanga
ambao Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliwakabidhi majukumu mbalimbali ikiwemo
daftari maalum la usajili wa madereva wote wa Bodaboda katika Mkoa wa
huo kwa ajili ya utambuzi na utaratibu mwingine wa kiutendaji kwa ajili
ya kuboresha huduma hiyo ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo ajaili za mara kwa mara.Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa Rukwa
No comments:
Post a Comment