Mheshimiwa Naomi Kaihula ni Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).Kabla hajawa Mbunge Mh Kaihula alikuwa Mwalimu wa Sekondari ya Tambaza kisha baadaye alijiendeleza Kimasomo, baadaye alichukua Shahada ya Uzamili(Masters degree) kisha akaajiriwa kama Lecturer wa moja ya vyuo vya elimu ya juu hapa nchini.
Pamoja na
CV hiyo fupi, mama huyu AMEOKOKA, na pia
ndiye mama mzazi wa Mwanamuziki wa hip Hop Gwamaka Kaihula au kwa jina
maarufu King Crazy GK ambaye alikuwa kiongozi wa kundi la EAST COAST.
"Nilibahatika kuwa mmoja wa wanafunzi wa mama huyu, nakumbuka
chuoni, moja kati ya vitu alivyokuwa akituambia ni kuwa Msifuatishe
Gwamaka 'G.K' nshapiga kelele sana arudi darasani asome yeye anakalia hayo hayo tu,
nawaambia nyie someni ipo siku mtamuajiri. Wakati mwingine aliwahi sema NAFANYA
MAOMBI SANA ILI GWAMAKA ABADILIKE asome kama nyinyi, haya ni moja kati ya maneno
mbayo siwezi yasahau,".
Wiki
moja
iliyopita Gwamaka Kaihula alitimiza ndoto ya mama yake aliyokuwa
akiitaka mtoto wake GK asome, G.K ametimu Shahada yake ya kwanza kutoka
chuo kikuu cha Tumaini Dar es Salaam Campus(TUDARCO), na hii ni baada ya
miaka
sita toka mama huyu atoe zile kauli, kumbuka wakati anasema hivyo
darasani
alikuwa akidai miaka mingi amekuwa akimuimbia mwanaye arudi shule lakini
wapi.Hapa
KIBIBLIA tunajifunza kitu kuwa kuna mambo mengine unaweza yaombea na
Kuyaombea
utashirikisha watu wataomba but yanaonekana kama bado hayaendi, good
thing ni
kwamba Mungu wetu ni mwaminifu HUFANYA.
Kwa
mtu yeyote aliyeokoka na mwenye mtoto atakuwa akielewa vizuri ni namna gani
mzazi unaumia pindi unapoona mtoto hajakaa sawa kitabia. Cha msingi hakuna
kukata tamaa ni kwenda mbele za Mungu bila kukoma na kwa wakati wake hufanya. Inawezekana
labda umekuwa ukiomba Mungu afanye jambo Fulani miaka nenda rudi, elewa MUNGU
wetu hajatupungukia wala hajalala, ni
Mwingi wa FADHILA atajibu tu tusipozimia ROHO.
http://hosannainc.blogspot.com/
http://hosannainc.blogspot.com/
kweli kabisaaa, mama amefanya kazi kubwa sana,umefanya vyema kutimiza ndito yake. ukimsikiliza mama hata mambo yako yataenda sawa.
ReplyDelete