Wasanii
wa Safari Lager Wezeshwa kutoka Kampuni ya Integrated Communications
wakicheza wakati wa Tamasha la kuelimisha wakazi wa jijini Arusha maeneo ya Tengeru kuhusu program ya Safari Lager Wezeshwa awamu ya pili leo.
Balozi wa Saafari Lager Wezesha, Faudhia Mohamed (kushoto) akiwaelimisha wakazi wa Tengeru jijini Arusha kuhusu program ya Safari Lager Wezeshwa awamu ya pili leo.
Wasanii wa Safari Lager Wezeshwa kutoka Kampuni ya Integrated Communications wakishambuia jukwaa.
***************************
KAMPUNI
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager kesho inatarajia
kuzindua rasmi msimu wa pili wa programu ya kuwaelimisha wajasiriamali
wa jijini Mwanza juu ya “Safari Lager Wezeshwa”.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam jana Meneja wa bia ya
Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema timu ya Mabalozi 15 wa ya
kuelimija jamii imeshawasili jijini Mwanza tayari kuanza kutoa elimu kwa
jamii ya wakazi wa Mwanza hasa wafanyabiashara ndogo ndogo na wa kati
juu ya programu ya Safari Wezeshwa.
Alisema
Shelukindo, timu hiyo ilianzia Mkoani Kilimanjaro na baadae ikahamia
jijini Arusha ikielimisha jamii ya Watanzania juu ya programu hiyo na
sasa kesho ni jijini Mwanza ambapo watafanyakazi katika viwanja vya
Igoma Standi kwa siku ya kwanza na siku ya pili watakuwa viwanja vya
Paseansi na baadae watahamia Shinyanga,Kahama na Tanga.
Programu hii
ilipata mafanikio makubwa, mwaka jana iliwawezesha wajasiriamali 54
waliofaulu vizuri vigezo kwa kuwapa mafunzo ya biashara na ruzuku za
vitendea kazi mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mia mbili.
Bwana Shelukindo alisema, “Safari Lager kwa mara ya pili inawaletea wamiliki wa biashara nafasi ya kukuza biashara zao na kujiimarisha wao binafsi na jamii inayowazunguka. “Safari Lager Wezeshwa”itatoa
ruzuku nyingine ya thamani ya shilingi milioni mia mbili, hii ni katika
harakati za kukuza na kuendeleza biashara za wajasiriamali zaidi
watakaoingia na kufuzu vigezo vya program hii”. Aliendelea kusema
kwamba, nia hasa ya Safari Lager ni kuwazawadia wajasiriamali ambao
wamejitahidi zaidi na kufikia mafanikio katika kazi wanazofanya kiasi
cha kuleta manufaa kwao na kwa jamii inayowazunguka”.Alifafanua kwamba
programu hii inawalenga wajasiriamali wadogo wadogo na sio
wafanyabiashara wakubwa. Alisisitiza zaidikwamba nia hasa ya programu
hiini kutoa hamasa kwa wajasiriamali
kote
Tanzania ili wajitahidi zaidi katika shughuli wanazofanya na pia
kuwazawadia wale watakaofaulu ili waweze kufikia ndoto zao. Kama
ilivyokuwa msimu uliopita, fedha hizi hazitolewi kama fedha taslimu kwa
watakaofaulu vigezo, zinatolewa kama vitendea kazi vitakavyomsadia
mjasiriamali kulingana na kazi anayofanya.
Shelukindo alimaliza kwa kuwapa changamoto wajasiriamali kujitahidi zaidi sio tu kwa ajili ya kujishindia ruzuku za programu ya“Safari Lager Wezeshwa” lakini
kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla. Aliwasihi wajasiriamali na
wafanyabiashara kwa ujumla kutega sikio kwa taarifa zaidi juu ya usajili
na kutembelea website yawww.wezeshwa.co.tz.
Bwana
Shelukindo alimaliza kwa kusema, “Tunatoa pongezikwa wajasiriamali kote
Tanzania, Safari Lager inatambua na kuthamini mchango wao mkubwa katika
maendeleo ya Taifa letu. Tunatoa shukrani zetu za dhati pia kwa
wanywaji wa Safari Lager, tunawaomba waendelee kuburudika na bia hii
inayoongoza Tanzania kwani ni mchango wao ndio unaofanya tunawawezesha
wajasiriamali wetu. Safari Lager ni bia kamili, inayodhihirisha mabingwa!.
No comments:
Post a Comment