Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 15, 2012

TIGO YASABABISHA KIZAZAA KWA WATEJA WAKE

Na Mwandishi Wetu

KUKATIKA kwa mawasiliano katika mtandao wa Tigo kwa wateja wake wote nchini kumezua kizazaa cha kuhaha kuwasiliana na ndugu zao na wengine kushindwa kutuma fedha kwa njia ya simu Tigo Pesa kutoka jana usiku hadi saa tano ya leo.

Ofisa Uhusiano Msaidizi wa Tigo, Tuli Mwaikenda alisema tatizo hilo limetokana na kukatika kwa umeme uliosababisha mfumo wa mawasiliano ya Tigo kukatika na kusababisha usumbufu mkubwa.

Msemaji wa Kitengo cha Mawasiliano wa TANESCO, Badra Masoud alikiri umeme kukatika na hiyo imesababishwa na mitambo ya gesi inayozalisha umeme katika kisima cha Songosongo mkoa wa Lindi kupokea gesi chini ya asilimia 50.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Fadhil Kilewo alisema kukatika kwa umeme kunatokana na uchakavu wa mitambo ya TANESCO.

1 comment:

  1. Τhiѕ website wаs... how dо уou say
    it? Relevant!! Fіnally I havе found something which helped
    mе. Thanks!Same Day Edit
    My web site :: Music Video

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...