Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 26, 2012

Dikteta ya Chekibudi kukimbiza soko la filamuNa Elizabeth John

MUIGIZAJI wa filamu nchini, Mohamed Nurdin ‘Chekibudi’ ameonekana kupanda katika soko la filamu baada ya kuachia filamu yake inayokwenda kwa jina la ‘Dikteta’, ambayo imeanza kufanya vizuri sokoni.

Filamu hyo mpya inayoonesha ukandamizaji wa familia, imekamilika na kuingizwa sokoni hivi karibuni, ambapo tayari imeanza kufanya vizuri katika  mauzo, katika baadhi ya maeneo ya jijini  Dar es Salaam, ikisambazwa na kampuni ya steps Entertaiment.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Chekibudi amesema, filamu hiyo ameiandaa ili kuonesha ukandamizaji uliopo baadhi ya familia katika maisha ya kila siku, na amefarijika kuona iko katika wakati mzuri sokoni.

Alisema baada ya kuangalia hilo, aliamua kuweka wazo lake katika filamu ili kuwafikishia ujumbe watu wengi zaidi na ikawa kama ni moja ya kazi za wasanii kuelimisha na kufundisha jamii.

“Unajua unapokuwa msanii unatakiwa kuwa mbunifu katika mambo mengi na ndiyo maana kila kukicha tunaangalia ni jinsi gani tutawakumbusha wenzetu matatizo ambayo yanaepukika,” amesema Chekibudi.

Chekibudi alishawahi kufanya vizuri alipokuwa katika kundi la sanaa la ‘Splendid’, na katika filamu hiyo ya ‘Dikteta’ amewashirikisha nyota wengine kama, Cojack, Philipo, Munira Sultan, Snura Mush, Coletha Reymond pamoja na nyota wengine.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...