Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 21, 2012

NDOA YA AUNT EZEKIEL YAINGIA DOSARI BAADA YA TETESI KUSAMBAA KUWA MUME WAKE ANASAKWA NA POLISI
BAADA ya ile harusi ya msanii maarufu wa filamu bongo Aunty Ezekiel kufungwa huku mastaa wakimsapoti shangwe, ishu nzito imeanza kujitokeza kuwa mume wa msanii huyo hawezi kuonekana kwenye ardhi ya bongo siku za usoni, kwa madai kuwa anatafutwa na jeshi la Polisi.

Upekuzi uliofanywa na mwandishi wetu wa kutaka kubaini kwa nini bwana harusi hakutaka kumaliza ishu hiyo mwenywe, ndipo taarifa hizo zilipobainika kuwa jamaa huyo kuna ishu nzito aliyoifanya bongo na ndiyo sababu kubwa ilimfanya asije hata kuonekana kwa wakwe zake.

Chanzo cha habari kilichozungumza namtandao huu kimedai kuwa awali kabisa kabla ndoa haijafungwa jamaa alitakiwa kuja nnchini lakini hakuweza kukubali kwa kujua kuwa anatafutwa na polisi na endapo akionekana atakuwa kwenye matatizo.

Mtu huyo aliongeza kuwa kuna uwezekana hata wanafamilia wa msanii huyo wakashindwa kumuona kabisa mwanaume huyo kwani ishu inayoendelea ni kwamba jamaa ameshatoa taarifa kuwa hawezi kuja nchini na mtu anayemtaka basi ni lazima apange safari amfuate.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...