Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 28, 2012

MFUKO WA MIKOPO USIO NA RIBA WAANZISHWA



DAR ES SALAAM, Tanzania
Akizungumza na vikundi vya akina mama hao, kwenye hafla ya uzinduzi wa Mfuko huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Chaurembo alisema mfuko huo utasaidia kukuza mitaji ya kina mama hao ambao ndiyo nguzo ya familia.
Alisema kuwa ameanzisha mfuko huo mahususi kwa akina mama kutokana na ukweli kwamba wao ndiyo wanaopambana na matatizo mbalimbali ya familia ikiwemo kusimamia afya na maendeleo ya watoto.
“Nilikuwa na uwezo wa kuanzisha mfuko kama huo kwa ajili ya vijana au hata wakina baba lakini nimeona wakina mama ndiyo wenye majukumu makubwa katika jamii yetu tofauti na sisi akina baba”alisema.
Aidha, Chaurembo alikabidhi sh 200,000 kila kikundi kati ya vikundi sita vilivyojitokeza kwenye hafla hiyo, ambapo aliwaasa vikundi hivyo vilivyopata mkopo huo, wakazitumie katika malengo waliyokusudia na si vinginevyo.
Alisema huo ni mkopo, kila kundi kitakachofanikiwa kumaliza mkopo huo kitaweza kupata mwingine zaidi yaw a awali.
“Fedha zipo kwa Ofisa Maendeleo wa kata hiyo, ni akina mama wenyewe kujipanga katika vikundi ili kupatiwa mafunzo ambayo yatawasaidia kuendesha biashara zao kwa ufanisi bila kubahatisha, hayo ndiyo masharti ya mkopo huu”alijinasibu.
Akizumzia mkopo huo kwa niaba ya wenzake, mmoja wa wanavikundi hivyo, Zena Said , alisema watahakikisha wanaitumia vyema fursa hiyo, bila kumuangusha diwani wao kwani hiyo ni mara ya kwanza kutokea katika kata hiyo kwa diwani kuanzisha mfuko kama huo, unaowalenga wanawake pekee.
Awali mgeni rasmi Peter Kirenge ambaye ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema hatua aliyochukuliwa diwani huyo, haifai kubezwa bali inapaswa kuigwa na viongozi mbalimbali ikiwa wa vyama vya siasa au hata wadau mbalimbali, kwa kutoa mikopo isiyokuwa na kero kama vile riba kubwa ambayo wakati mwingine husababisha akina mama hao kushindwa kulipa na kunyang’anywa mali zao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...