Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 26, 2012

MUIGIZAJI JOHN STEPHANO MAGANGA AFARIKI, KUZIKWA JUMANNE MAKABURI YA KINONDONI


  JOHN MAGANGA enzi za uhai wake.
TASNIA ya filamu nchini Tanzania, imefikwa na msiba mwingine Mkubwa wa Msanii wa Filamu, John Stephano Maganga aliyefariki jana katika Hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa viongozi wa Wasanii zinasema kuwa Mipango ya mazishi inafanyika Nyumbani kwao Mwananyama A jirani na Kopakabana Bar  jijini Dar es Salaam.
Marehemu John anaetarajiwa kuzikwa siku ya jumanne Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam, alianza kujiingiza katika sanaa ya uigizaji mwaka 2001 chini Thea na Deo Shija na ilipofika mwaka 2008 alianza kuigiza filamu na hadi mauti yanamfika alikuwa njiani kutoa Filamu yake.
Aidha Wasanii wote wanataarifiwa kufika katika Kikao Maalum Nyumbani kwa John Stephan oleo Saa tisa alasiri kwaajili ya kupanga mikakati, ya mazishi.
Pia Mtanzania yeyote atakae guswa na Msiba huu anaweza kutuma Rambi Rambi zake kupitia Namba ya Tigo Pesa za 0715541714 au 0718951355

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...