Diwani wa Kata ya Dodoma mjoni, David Madole akimkabidhi Kikombe nahodha wa timu ya Atlantic mara baada ya kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya Safari Pool ngazi ya mkoa, Mkoa wa Dodoma yaliyo malizika mjini hapo mwishoni mwa wiki.Wengine ni wachezaji wa Klabu hiyo.
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya mchezo wa pool ya Atlantic yenye makazi yake Majengo Mjini
Dodoma, ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya pool ya 'Safari
Lager National Pool Championships 2012' baada ya kuibamiza klabu ya
Florida yenye makazi yake Barabara ya Bahi, 13-8 katika mchezo wa
fainali wa mashindano hayo ngazi ya mkoa yaliyofanyika katika Klabu ya
Atlantic mjini Dodoma.
Atlantic ilitwaa ubingwa huo na kujinyakulia fedha taslimu Sh.700,000 na
Kikombea mbapo pia kuwa wawakilishi wa mkoa huo katika fainali za
Kitaifa zitakazofanyika Septemba 26 mwaka huu mkoani Mwanza kwa
kushirikisha vilabu 16 ambavyo vitakuwa mabingwa kwenye mikoa yao.
Florida ilikamata nafasi ya pili na kuzawa kitita cha shilingi 350,000
na mshindi wa tatu katika mashindano hayo ni Klabu ya Tiger yenye makazi
yake eria C, ambao walizawadiwa shilingi 200,000 na wanne ni klabu ya
Car Wash ya Bara bara ya Bahi ambao walizawadiwa shilingi 100,000.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja “Singles” (wanaume), Abdu Forty kutoka
klabu ya Florida alitwaa ubingwa kwa kumchapa Athuman Gora wa klabu ya
White Horse 4-0, na kujinyakulia kitita cha shilingi 350,000 ambapo Abdu
Forty alikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa shilingi 200,000, wakati
Mohamed Jafari wa Klabu ya Atlantic alikamata nafasi ya tatu na
kuzawadiwa shilingi 150,000.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja “Singles” (wanawake),Monica Simule
alitwaa Ubingwa na kuzawadiwa Shilingi 250,000/= na nafasi ya pili ni
Happy Mkumbo.
Zawadi kwa washindi wote zilikabidhiwa na Diwani wa Dodoma Mjini, David
Madole ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele cha mashindano hayo
katika Mkoa Dodoma
No comments:
Post a Comment