Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 10, 2012

KHADIJA MNOGA AKA KIMOBITEL AWABIP WAPENZI NA WASHABIKI WA EXTRA BONGO KWA WIMBO WAKE MPYA ALIOUPA JINA LA “MGENI” NDANI YA MEEDA.


Kimobitel akiimba wimbo wake aliyeutunga mwenyewe unaojulikana kwa jina la “MGENI” ndani ya Meeda Sinza Usiku wa kuamkia leo.
Khadija Mnoga “Kimobitel” hivi majuzi alitangaza rasmi kuihama Bendi yake ya Twanga Pepeta ambayo aliitumikia kwa miezi kadhaa na kuhamia Extra Bongo, sababu za kuhama Kimobitel alisema ameamua kurudi Extra Bongo kwa sababu kuna mipango yake ambayo aliianzisha kwa hiyo amekuja kuimalizia kama wimbo ambao aliwahi kuimba wakati anaiimbia bendi hiyo unaotambulika kwa jina la “MJINI MIPANGO” kwa hiyo ameamua kurudi kuja kuikamilisha mipango hiyo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki amesema KIMO KIMO kama wengine wanavyomuita atatambulishwa rasmi siku ya Ijumaa ya tarehe 14/09/2012 katika ukumbi wao wa nyumbani New White House uliyopo Kimara Korogwe jijini Dar es salaam.
Kulia ni Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Choki akiimba wimbo mpya wa Kimobitel ndani ya Meeda Sinza
Safu ya wanamuziki nguli wa Extra Bongo walioimba wimbo mpya wa Kimobitel (Mgeni) wakiongozwa na Ally Choki wa pili kutoka kushoto, wa kwanza kulia ni Rogert Hega Katapila, anafuatiwa na Banza Stone na Kushoto ni Kimobitel.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...