Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa Tuzo ya Uongozi Bora wa sera ya
Kilimo na Chakula toka kwa Bw. Ajay VAshee, Makamu Mwenyekiti wa asasi
isiyo ya kiserikali inayohusika na sera za kilimo na chakula na
Maliasili n ijulikanayo kama Food,
Agriculture and Natural Resources Policy (FANRPAN) katika hoteli ya
White Sands jana Septemba 5, 2012. Anayeshuhudia kulia ni Katibu
Mtendaji wa FANRPAN) Dkt Lindiwe Sibanda. Tuzo hiyo, ambayo hutolewa kwa
kiongozi aliyefanya juhudi kuhakikisha kuwepo kwa sera bora za kilimo
na chakula nchini kwake, ilichukuliwa na Malkia Ntombi Indlovukazi wa
Swaziland mwaka jana, wakati Rais Hifikepunye Pohamba alitunukiwa mwaka
2010, Rais Armando Emilio Gwebuza mwaka 2009 na Rais wa Malawi, Hayati
Bingu Wa Mutharika, aliipokea mwaka 2008.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia baadhi ya ng'ombe anaowafuga kwa
kufuata njia za kisasa kwenye shamba lake kijijini kwake Msoga,
Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, leo Septemba 6, 2012.
No comments:
Post a Comment