Kamanda
wa polisi mkoa wa Kipolisi wa kinondoni Charles Kenyela anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika pambano la ngumi la kutetea ubingwa Afrika
mashariki na kati kati ya bondia Mtanzania Thomas Mashali na Bernad
Mackoliech wa Kenya Jumamosi katika Ukumbi wa Friends Corner Manzese.
Akizungumza
na waandishi wa habari mratibu wa pambano hilo Aisha Mbegu alisema
wameamua kumualika kamanda Kenyela ili kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo
kutoa Elimu ya Ulinzi shirikishi na kwa kutambua mchango wa jeshi la
polisi kudumisha amani katika michezo.
“
Jeshi la polisi ni wadau wetu wakubwa katika michezo hasa ngumi na
mchango wao umekuwa ukionekana kwani sasa hakuna vurugu zinazojitokeza
katika mapambano yeyote ya ngumi yanayofanyika tofauti na Miaka ya Nyuma
ambapo Ngumi ilikuwa Watoto hawawezi kwenda kuangalia,”alisema Aisha.
Aisha
alisema katika pambano la awali ambalo lilifanyika katika Ukumbi wa
Friend corner hakukuwa na vurugu na idadi ya watoto na wanawake
kuangalia ngumi imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na nhivyo kutoa
hamasa kwa wazazi na watoto kupenda mchezo huo.
Mbali na Kenyela Mbunge wa Kinondoni Iddi Azan na Mbunge wa ubungo John Mnyika wamealikwa ili kushuhudia vipaji vya vijana wa kinondoni katika Ngumi.
Bondia
Mackoliech anatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari leo (Alhamisi)
katika Uwanja wa Karume na Ijumaa wanatarajiwa kupima Uzito saa Nne
asubuhi katika Ukumbi wa Friends Corner Manzese .
No comments:
Post a Comment