Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa amevipatia vukundi saba vya Vikoba
vilivyopo Wilayani Monduli,kiasi cha shilingi milioni nane kwa ajili ya
kuendeleza shughuli zao.Lowassa amesema yeye ni mkereketwa mkubwa wa
Vikoba huku akisisitiza kuwa ni chachu ya maendeleo na kumkwamua
mtanzania kutoka katika umasikini. kila kikundi kimepata shilingi
millioni moja ambapo kikundi kilichofanya vizuri kimeongezewa shilingi
millioni moja zaidi.Pichani ni Mh. Lowassa akikabidhiwa zawadi na
mwenyekiti wa Vikoba Kijiji cha Monduli Juu,Dawson Kaaya wakati viongozi
wa vikundi hivyo walipomtembelea nyumbani kwake Monduli.
Mmoja wa viongozi wa vikundi vya vikoba Kijiji cha Monduli Mjini akisoma risala mbele ya Mh Lowassa.
Baadhi ya wanavikoba wa Monduli Mjini wakimsikiliza Mh. Lowassa.
Mhe Edward Lowassa akipewa zawadi na
Bi Arafa Ismaild kutoka katika vikundi vya Vikoba Monduli mjini ambao
walikwenda kumtembelea nyumbani kwake. Kushoto kwa Mhe ni Bw. Dawson
Kaaya ambaye ni Mwenyekiti wa Vikoba Monduli Mjini.
No comments:
Post a Comment