Kutokana Nchini Nyingi za Afrika
Ikiwemo Tanzania Kulazimika Kuingia Kwenye Mfumo Mpya Wa Kurushia
Matangazo ya televisheni wa digitali na kutoka Kwenye mfumo wa Zamani wa
Analogia na Kupelekea Kuleta sintofahamu kwa wakazi wengi wa Tanzania
kutokana na kutokuwa na Ufahamu japo kidogo juu ya Mfumo huu na Vifaa
vinavyotumika katika Mfumo huu wa Digitali katika kupokea mawimbi hayo
ndipo Lukaza Blog Imeamua kila Jumatatu itakuwa inaleta Somo Juu ya
Mfumo Mzima Wa Digitali ambapo katika Mfumo huu Tutaangalia Juu ya
Ving'amuzi na Satelite na tutaangalia Juu Ya Mfumo Mzima Wa Satelite na
Upokeaji wa Mawimbi ya Satelite.
Kutokana Na Watanzania Wengi
kutokuwa na Uelewa Juu ya Vitu hivi Ndipo Lukaza Blog Imeamua Kuleta
Somo hili la Digitali na Somo Hili litakuwa linatolewa Kila Jumatatu
Kupitia wataalamu wetu wa Mambo ya Digitali na Mifumo Ya satelite na Juu
ya Aina Gani ya Ving'amuzi inafaa katika Ukanda wetu huu Wa Tanzania.
Kaeni Mkao wa Kula Kuanzia Jumatatu ya Kesho somo letu litakuwa Juu ya Mawasiliano ya Satelite, Satelite ni nini?,Aina Za Satelite? ,Na Satelite za Mawasiliano.
Karibu
Katika Somo hili la Mawasiliano ya Satelite Na matarajio yetu Kuwa
Wasomaji wetu Mtapata Uelewa juu ya Mfumo Huu na kupelekea Kujua Ni Nini
na Nini Kinahitajika Katika Ulimwengu huu wa Digitali
Lukaza Blog Kwa Kuona Umuhimu wa
Kupata elimu hii ya Mawasiliano ya Satelite ambao ndio Mfumo wa Digitali
wenyewe Basi tumeamua Kuwaletea Wasomaji wetu Somo hili Kwa
Kushirikiana na Wataalamu wetu Wa Maswala ya Mawasiliano ya Satelite
ambayo ndio Mfumo Mzima Wa Digitali ili kusudi Watanzania wote tupate
elimu ya kutosha katika swala zima la Mfumo wa Digitali.
Somo hilo litakuwa linapatikana kupitia anuani hii chini
http://josephatlukaza.blogspot.com
Imetolewa na
- Josephat Lukaza -
- Lukaza Blog Admin -
- http://josephatlukaza.blogspot.com -
No comments:
Post a Comment