Bondia Benard Mcociech wa Kenya akipimwa afya na dkt madorina
Mtanzania Thomas Mashali na Bernad
Mackoliech kutoka nchini wa Kenya wakitambiana mara baada ya kupima
uzito leo katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam.
---
Dar es Salaam.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi wa
kinondoni Charles Kenyela anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano
la kutetea ubingwa Afrika mashariki na kati kati ya bondia Mtanzania
Thomas Mashali na Bernad Mackoliech kutoka nchini wa Kenya Jumamosi
katika Ukumbi wa Friends Corner Manzese.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo wakati mabondia hao wakipima uzito, mratibu wa pambano hilo Aisha
Mbegu alisema wameamua kumualika kamanda Kenyela ili kuhakikisha
wanatumia nafasi hiyo kutoa Elimu ya Ulinzi shirikishi na kwa kutambua
mchango wa jeshi la polisi kudumisha amani katika michezo.
“Jeshi la polisi ni wadau wetu
wakubwa katika michezo hasa ngumi na mchango wao umekuwa ukionekana
kwani sasa hakuna vurugu zinazojitokeza katika mapambano yeyote ya ngumi
yanayofanyika tofauti na Miaka ya Nyuma ambapo Ngumi ilikuwa Watoto
hawawezi kwenda kuangalia,” alisema Aisha.
Aisha alisema katika pambano la awali
ambalo lilifanyika katika Ukumbi wa Friend Corner hakukuwa na vurugu na
idadi ya watoto na wanawake kuangalia ngumi imekuwa ikiongezeka siku
hadi siku na hivyo kutoa hamasa kwa wazazi na watoto kupenda mchezo huo.
Mbali na Kenyela Mbunge wa Kinondoni
Iddi Azan na Mbunge wa ubungo John Mnyika wamealikwa ili kushuhudia
vipaji vya vijana wa kinondoni katika Ngumi.
No comments:
Post a Comment