Mke
wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni, akizungumza na wanachama wa
Nungwi Saccos, wakati alipofika kutembelea kikundi cha Ushirika cha
Kinamama, kilichopo Tawi la CCM Nungwi, kwa ajili ya kukabidhi ahadi ya
mchango wa mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma
kikwete, kiasi cha Sh. 2,000,000/- kwa kikundi hicho, jana.
Mke
wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni, Mkurugenzi Tiba Dr. Salhia
Ali Muhsin na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha
Suleiman Iddi, wakifurahia na kuangalia vifaa mbali mbali walivyovitoa
kwa ajili ya Hospitali ya Kivunge iliyoko Wilaya ya Kaskazini “A”, jana.
Mke
wa Rais wa Zanzibar, Mwanamwema Sehni, akikabidhi Viti vya Wagonjwa kwa
Mkurugenzi Tiba Wizara ya Afya Dr. Salhia Ali Muhsin, wakati
alipotembelea katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A, jana.
Mke
wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni, akionyesha kitita cha fedha,
kuashiria utekelezaji rasmi wa ahadi ya Mke wa Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Slma Kikwete ya kukabidhi mchango wa shilingi
2,000,000/- Ushirika wa Nungwi Saccos.
Mke
wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni, akikabidhi mchango wa
shilingi 2,000,000/- kwa kiongozi wa kikundi cha Nungwi Saccos, ikiwa ni
utekelezaji wa ahadi ya Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mama Slma Kikwete aliyoitoa mwezi Mei mwaka 2010.
Akina
mama wa Ushirika wa Nungwi Saccos wakishangiria mchango wa shilingi
milioni 2,000,000/- zilizotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama
Mwanamwema Sheni ambazo ziliahidiwa na Mke wa Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete wakati akiizindua Nungwi Saccos
Mwaka 2010.
*****************************************
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuunga
mkono juhudi za Wananachi wake katika kuhakikisha changamoto pamoja na
matatizo yanayowakabili Wananchi hao yanatekelezwa.
Utekelezaji huo utaendelea kufanywa kwa pamoja kati ya Serikali, Taasisi na mashirika hisani kwa kuwajumuisha na wananchi wenyewe kutegemea nguvu na uwezo unavyoruhusu kiuwezeshaji.
Mke
wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni akiambatana na Mke wa Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman pamoja na wake wa
Wawakilishi na Wabunge wa CCM alitoa kauli hiyo mara baada ya kukabidhi
misaada wa mbali mbali kwa ajili ya Hospitali ya Kivunge iliyoko Wilaya
ya Kaskazini A.
Msaada
huo uliogharimu jumla ya Shilingi Milioni Sita { 6,000,000/- }
ukijumisha magodoro 16, Vitanda 16, Mito 16, Viti vya wagonjwa vitatu,
Sabuni unafuatia ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi aliyoifanya katika Hospitali hiyo mwaka jana na kuelezewa
changamoto kadhaa zinazoikabili Hospitali hiyo ikiwemo uchakavu na uhaba
wa Vitanda na Magodoro.
Mama
Mwanamwema Sheni aliwataka Wananachi na wafanyakazi wa Kituo hicho
kuendelea kuwa wastahamilivu licha ya kwamba matatizo hayo ni kilio cha muda mrefu.
“ Upungufu wa Vifaa umekuwa ukizikumba Taasisi na majengo kadhaa ya Umma, Jamii na hata binafsi lakini cha kuzingatia zaidi ni ustahamilivu na kutafuta mbinu mbadala za kukabiliana na matatizo hayo”. Alisisitiza Mama Mwanamwema Sheni.
Mwenyekiti
huyo wa Umoja wa wake wa Viongozi wa CCM aliikumbusha Jamii kuendeleza
upendo na mshikamano kwa lengo la kulijengea hatma njema ya Amani na
Utulivu Taifa hili.
Akipokea
Msaada huo Mkurugenzi Tiba Wizara ya Afya Dr. Salhia Ali Muhsin
alimpongeza Mama Mwanamwema Sheni pamoja na Wanachama wa Umoja huo wa
Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM kwa juhudi zao za kusaidia
maendeleo ya Jamii na Hasa wakilenga zaidi akina mama.
Baadaye Mama Mwanamwema Sheni alikabidhi Mchango wa Shilingi Milioni
mbili { 2,000,000/- } kwa ajili ya Nungwi Saccos ili kutekeleza ahadi
iliyotolewa na Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama
Salma Kikwete.
Ahadi hiyo ilitolewa na Mama Salma Kikwete wakati akiizindua Nungwi Saccos Tarahe 11 mwezi Mei Mwaka 2010 hapo katika Majengo ya Skuili ya Amali yaliyopo Mkokotoni Mkoa wa Kaskazinin Unguja.
Mama mwanamwema Sheni katika kuunga mkono juhudi wanazochukuwa wanachama
hao za kujiletea maendeleo yeye pamoja na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi wameahidi kuchangia Mabati kwa
ajili ya Uwezekaji wa Jengo la Ushirika huo.
Aliwataka
akina mama wote Nchini kudumisha mshikamano utakaosaidia Taifa
kuendelea kupiga hatua kubwa zaidi za kiuchumi na ustawi wa Jamii.
Naye Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha
Suleiman Iddi akitoa nasaha zake katika hafla hiyo alieleza misaada
hiyo ni miongoni mwa utaratibu ulioandaliwa na Umoja wa wake wa
wawakilishi na Wabunge wa CCM.
Mama
Asha alisema kwamba michango hiyo wakati wote hulenga katika kuunga
mkono harakati zao za kiuchumi bila ya kuingiza itikadi za Kisiasa
ambazo zimekuwa na utaratibu wa kulenga watu na makundi Maalum.
Akitoa Taarifa fupi Katibu wa Ushirika
huo wa Nungwi Saccos Bibi Siti Ali Makame kwa niaba ya Wanachama
wenzake wamewapongeza Viongozi wa Serikali na Taasisi zake kwa juhudi
kubwa inazochukuwa katika kuona kundi kubwa la wanawake linakomboka
katika dimbwi kubwa la umaskini.
Bibi
Siti alisema wanachama wa kikundi hicho wametoa shukrani za pekee kwa
Taasisi ya Kimataifa ya misaada ya Action Aid kutokana na jitihada zake
zilizochangia kuanzishwa kwa ushirika huo wa Nungwi Saccos.
Mke
wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni, Mke wa Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi pamoja na wake wa wawakilishi
na wabunge wa CCM walipata wasaa wa kumtembelea Muasisi wa Chama cha
Afro Shirazy Party Bibi Kombo Juma.
Ujumbe huo ulimjulia hali Muasisi huyo hapo nyumbani kwake katika Kijiji cha Nungwi kiliopo Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja
Imetolewa na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
3/1/2013.
No comments:
Post a Comment