Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, April 3, 2013

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO YATIMA


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti Muzdalifa,Sheikh Abdalla Hadhal,alipoangalia maonesho ya picha   mbali mbali wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Yatima katika Ukumbi wa Salama Bwawani leo, maadhimisho hayo yamefanywa na Shirika la I.H.H la nchini Uturuki kwa ushirikiano na Jumuiya ya Muzidalifa ya hapa Zanzibar inayoshuhulika kna Mayatima,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi kutoka kwa Mtoto  Hinaina Said Khalfan,wakati wa sherehe za siku ya Mtoto yatima zilizofanyika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel  leo Mjini Zanzibar,shirika la misaada la I.H.H la Uturuki,kwa Ushirikiano na jumuiya ya Muzdalifa ya hapa Zanzibar kwa pamoja wamefanikisha kufanyika kwa sherehe hizo.

 Watoto Yatima waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Mtoto Yatima,wakiwa katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar,zilipofanyika sherehe hizo,kwa ushirikiano wa jumuiya ya Muzdalifa na shirika la misaada la I.H.H la Nchini Uturuki leo na kuhudhuriwa na wananchi na Viongozi mbalimbali.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea risala kutoka kwa Nasra Suleiman Abdalla,wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake wakati wa Sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto Yatima katika ukumbi wa Salama bwawani Mjini Zanzibar leo,maadhimisho hayo yamesimamiwa na jumuiya ya Muzidalifa na Shikika la misaada la I.H.H la Nchini Uturuki,(kushoto) makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif,Balozi wa Uturuki Nchini Ali Daudi Gul,na  Waziri wa Katiba na Sheria,Abubakar Khamis Bakary,(kulia)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...