Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 13, 2013

GrandMalt yajitokeza kudhamini Uhuru Marathon


Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika leo kwenye Ukumbu wa Idara ya Habari-Maelezo,wakati wa kutangaza udhamini wa Mbio ya Uhuru Marathon.Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mbio za Uhuru Marathon Tanzania,Innocent Melleck
Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mbio za Uhuru Marathon Tanzania,Innocent Melleck (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo juu ya udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha GrandMalt ambapo kimetoa jumla ya shilingi milioni ishirini (20,000,000).kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah.

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha GrandMalt imejitokeza kudhamini mbio ndefu za Uhuru, Uhuru Marathon, kwa kiasi cha Sh milioni 20.
Akitangaza udhamini huo jijini Dar es Salaam jana, Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah alisema, wameona ni vyema kudhamini mbio hizo kwani zina lengo zuri zaidi la kuimarisha umoja, amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
Naye Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck aliwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo ambazo zina nia kubwa ya kutukumbukusha wajibu wetu wa kutunza na kulinda amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu.
Mbio hizi zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam hapo Desemba 8, mwaka huu ambapo zitaanzia na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders club.
Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kushiriki mbio hizi, huku wabunge zaidi ya 100 wakiongozwa na Spika Anne Makinda wakiwa wamejisajili kwa ajili ya kushiriki.
Mbio hizo zimegawanywa katika makundi makuu manne ambayo ni kilomita 3 kwa ajili ya viongozi, kilomita 5 kwa watu wote na kilomita 21 na 42 ambazo ni maalum kwa wakimbiaji nguli.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...