Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 14, 2013

Promota wa muziki awekewa ngumu Jijini Koloni,Ujerumani,kisa FFU na washabiki wao!





Ukiwataka FFU lazima uweke ulinzi mkali 

Promota wa muziki awekewa masharti magumu na serikali ya jiji la Koloni,

Promota wa muziki jijini Koloni Bw.Peter Betram (mjerumani),amejikuta akiwekewa masharti magumu katika juhudi zake za kutaka kuandaa onyesho kubwa la muziki katikati ya jiji la Koloni,nchini Ujerumani,kwa mda wa miaka miwili sasa poromota huyo amekuwa akilalamikia almashauri ya jiji kubwa la koloni kwa kumwekea ngumu katika kuandaa onyesho la muziki.

Kuanzia mwaka 20012 aliambiwa apeleke orodha ya bendi anazohitaji kuzipandisha jukwaani,baada ya kuonekana jina la bendi ya Ngoma Africa katika orodha hiyo,serikali ya jiji imemwagiza mtayarishaji wa onyesho hilo lazima akubali kuingia gharama za ziada kwa ajili ya ulinzi kutoka na msongamano wa washabiki,pia kapewa sharti lingine lazima onyesho hilo liwe nje ya mji sio kitovuni mwa jiji,kutokana na kuepuka msongamano wa washabiki wa Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni yenye tabia za kuwadatisha akili washabiki wake.

Poromota amejikuta akivimba macho na kutojua nini? cha kufanya. 
Wadaku walipo mtafuta kiongozi wa Ngoma Africa band kamanda Ras Makunja kutaka kupata mtazamo wake,kamanda alijibu kuwa kikosi chake kipo tayari tayari na wakati wowote ule watakapoitwa na poromota huyo,Ras Makunja alikili kuwa muda wa miaka miwili Poromota amekuwa akiwapigia simu,na bendi ipo tayari kama matayarisho yatakamilika alisema Kamanda Ras Makunja,

Mdodosa habari alipo hoji swala la kulikoni kamanda kumiliki bundi katika himaya ya  "Anunnaki Empire" Kamanda Ras Makunja kakata simu..!!! sijui kama aliishiwa chaji au aliondoka ki - FFU kwa mwendo wa kasi !? tu Any way tuwatafute kambini kwao  www.ngoma-africa.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...