Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 7, 2013

WATOTO WAHITIMU KIDATO CHA NNE

Na Peter Mwenda

WAHITIMU wa Shule za Sekondari na Vyuo vikuu nchinin wameshauriwa kutokata tamaa kutokana na uhaba wa ajira nchini bali waendelee kujishughulisha kwa kufanya kazi za ubunifu.

Hayo walisema jana Dar es Salaam na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa DAr es SAlaam, Bw. John Guninita kwenye mahafali ya Kidato cha Nne kwa Wanafunzi waliohitumu masomo ya Kidato cha Nne Katika Shule ya Sekondari ya Dkt. Didas Masaburi iliyocho Chanika Dar es Salaam.

Bw. Guninita alisema tatizo la kukosekana kwa ajira nchini ni kubwa lakini linaweza kutatulika endapo wahitimu wakiacha kusubiri ajira za Serikali badala ya kubuni njia ya kuendesha maisha yaokutumia akili waliyonayo.


Alisema Serikali ilitoa fursa kwa watanzania wenye uwezo wa kufungua shule wafanye hivyo na matokeo yake kuna shule ngingi za binafsi ambazo zinachangia kupatikana kwa elimu bora kama ya Dkt. Didas Masaburi ambayo inatoa vijana wengi wenye vipaji kwenda kidato cah nne, sita na Chuo Kikuu.

"Shule zaidi ya asilimia 95 zinamilikiiwa na Serikali lakinin kutokana na ongezeko la watu, serikali pekee isingeweza kukidhi mahitaji ya elimu nchini imetoa nafasi kuanzishwa kwa shule binafsi nchini" alisema Bw.Guninita.

Alisema vijana wanaohitimu mafunzo na kukata tamaa ya kukosa ajili baadhi yao wanajiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya na ngono zembe zinazosababisha matukio ya vifo vya kutisha vinavyotokea nchini.

Katika mahafali hayo ya saba ya shule ya Sekondari, Dkt. Didas Masaburi wanafunzi waliomaliza masomo yao waliomba Serikali kutoa vifaa kwa shule binafsi ambazo zinafanya vizuri katika ufundishaji.

Mkuu wa Shule hiyo, Bw. Michael Owiti alisema wanashirikiana vizuri na wazazi kuhakikisha mwanafunzi anayeiungia kusoma katika shule hiyo anapata elimu ya kutosha ili mwisho wa simu akumbuke kuwa elimu aliyonayo inatokana juhudi za shule hiyo kuwalea kwa lengo la kuishi maisha bora baadaye.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...