Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 11, 2013

MATAPELI WACHEZEA KICHAPO KUTOKA KWA WAKAZI WA SEGEREA MARA BAADA YA KUFANYA JARIBIO LA UTAPELI NA KUSHTUKIWA


 Wakazi wa mtaa wa migombani kata ya segerea wakiwahoji matapeli (hawapo pichani) ambao walikua wakijaribu kumfanyia utapeli dada mmoja na hatimaye kushindwa kutimiza lengo lao mara baada ya dada huyo kushtukia mbinu zao na kuomba msaada kwa wananchi na ndipo hapo walipotiwa nguvuni na kupelekwa katika ofisi za serikali ya mtaa wa migombani
 Matapeli (mwenye shati la draft) wakipewa kichapo mara baada ya kushindwa kujibu maswali ya wananchi waliowakamata leo katika kituo cha daladala cha Segerea
 Mmoja wa watumishi wa serikali ya Mtaa wa Migombani Kata ya segerea Mfaume (wa kwanza kushoto Mwenye fulana ya njano) akijaribu kuwakata wananchi hao kujichukulia sheria Mikononi mara baada ya kuwatia nguvuni matapeli hao leo katika kituo cha daladala cha Tabata Segerea
 Mmoja wa matapeli akijizuia kichwani mara baada ya wananchi wenye hasira kali wakiendelea kushusha kipigo kitakatifu, katika tukio la kujaribu utapeli lililotokea muda mfupi katika kituo cha daladala cha segerea mwisho 
 Hapa tapeli wa pili (aliyeinamishwa kichwa) akiendelea kupokea maumivu kutoka kwa wakazi wa segerea mara baada ya kukamatwa wakati wakitaka kujaribu kutapeli 
 kipigo kikiendelea kutolewa kwa matapeli hao

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...