Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 21, 2013

TUZO KUTOLEWA KWA WALIOTOA MCHANGO KATIKA SEKTA YA AFYA NOVEMBA 23,

NOVEMBA 23, mwaka huu, viongozi mbalimbai watapewa tuzo za kutambua
mchango wao katika kuboresha afya ya mama na mtoto.

Tuzo hizo zimeandaliwa na Taasisi ya Madakt
ari Waliosoma Vyuo Vikuu
nchini (THPI), na miongoni watakaopewa tuzo ni Rais Jakaya Kikwete,
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu
wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mke wa Rais, Salma Kikwete na
Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi

Kuhusu THPI, ilianzishwa mwezi Machi, 2009 na madaktari 12, na

Mkurugenzi  wa taasisi hiyo, Dk. Telesphory Kyaruzi, anasema wanaamini
wakiwa wengi, watahudumia
watu wengi na jamii kubwa zaidi.

Anasema, hadi sasa taasisi ina madaktari  wanachama

zaidi ya 120 ambao wamesambaa nchi nzima.

"Lengo kuu la taasisi yetu ni kushiriki katika kuhamasisha uboreshaji huduma

za afya nchini na kushiriki kikamilifu katika kutoa huduma bora za afya kwa
watanzania,"anaongeza.

Madaktari hao ni wale walioamua kubaki nchini badalayakukimbilia nje

ya nchi kufanya kazi...kwa kifupi ni madaktari wazalendo.

"Tuliamua kubaki nchini badala ya kwenda nchi za nje kutafuta maslahi mazuri

zaidi kwa sababu ya uzalendo juu ya nchi yetu.

"Dira ya taasisi yetu, tunaona watanzania wenye afya bora, huduma bora , na

miundombinu bora katika kutoa huduma za afya nchini .
Katika taasis yetu  nguvu yetu ni umoja;  wote ni sawa, kila mtu ni muhimu
na kila mtu ni kiongozi.  Nguvu yetu ni matumaini,"anaongeza.

Dk. Kyaruzi anasema ili kuwa na madaktari wengi sehemu mbalimbali

nchini wanaotoa huduma za afya,  taasisi imeanzisha Idara ya
Uendelezaji Madaktari Vijana inayoratibu
Mtandao wa Madaktari Vijana Nchini, ambao ni Madaktari Wanafunzi( Medical
Students), Intern Doctors, na Madaktari wanaoanza kazi ili kuwajengea uwezo
kitaaluma.

Aidha, katika kutatua matatizo ya afya nchini, anabainisha kuwa

wanaongozwa na mpango mkakati.

Katika mpango wa mwaka 2011/2014, taasisi imejielekeza

katika kutekeleza malengo ya Milenia, lengo la nne na tano, afya ya
mama na mototo. Na
kufikia lengo la kupunguza vifo vya akina mama kwa 75% ifikapo mwaka 2015.

Katika kutekeleza jukumu hili muhimu, taasisi imeanzisha kampeni ya kitaifa

ya Saidia Mama Mjamzito Ajifungue salama, ili kupunguza vifo vya mama na
mtoto.

Kutokana na taarifa za jarida la umoja wa mataifa , Global Health and

Deplomacy, duniani kina mama  wajawazito 368,000 wanafariki kila
mwaka, nafasi ya mama mjamzito kufa ni mara 100 zaidi katika nchi zenye
idadi kubwa ya vifo vya akina mama vinavyotokana na ujauzito.

Akifafanua hilo, Dk. Kyaruzi anasema kuwa ni nchi 21 tu duniani ziko

kwenye hatua sahihi katika kufikia malengo ya millennia ifikapo mwaka
2015.

"Vifo vya mama wajawazito nchini kwa mwaka 2005 vilikuwa ni  578, kwa vizazi

hai 100,000,  na kufikia 454 kwa  vizazi hai 100,000 kwa mwaka 2012.

"Pia vifo vya watoto chini ya miaka mitano vilikuwa 122 kwa

watoto hai 1,000 mwaka 2004 mpaka 81 kwa watoto hai 1,000 mwaka 2012. Na
vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja ilikuwa 68 kwa watoto hai 1,000 kwa
mwaka 2004 mpaka 51 kwa watoto hai 1,000 kwa mwaka 2012,"anasema.

Kutokana na juhudi kubwa za wadau, anasema wamefanikiwa kumepunguza

idadi ya vifo vitokanvyo na ujauzito na vifo vya watoto
wachanga,   lakini lazima jitihada za kupunguza vifo vya mama na watoto
ziedelee kwa nguvu kubwa zaidi.


Ili kutekeleza kampeni ya Saidia Mama Mjamzito ajifungue Salama, anasema taasisi

ilifanya utafiti wa awali,  na kubaini upungufu wa damu ni namba moja,
ikifuatiwa na kifafa cha mimba,

Aidha ni asilimia 50 tu ya  wajawazito wanaorudi kujifungua katika

vituo vya afya, upungufu wa mindombinu na maambukizi ya Kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto ni changamoto kwa uzazi salama.


"Kupitia kampeni tunahamasisha  wananchi kuchangia damu ili kuokoa

maisha ya wajawazito wanaohitaji  kwa dharura na kuhamasisha kina baba
kushiriki katika afya ya uzazi ikiwa ni pamoja na kuwasindikiza
kliniki ili kujua dalili za hatari wakati wa ujauzito na kujiandaa
kujifungua.

"Kuongeza uwezo wa miundombinu katika utoaji huduma kwa mama

wajawazito ambayo ni matumizi ya simu kufuatilia mama mwenye dalili za
hatari
kupitia rafiki kliniki mpaka anajifungua salama, kujenga wodi na vyumba vya
dharura (ICU) na Upasuaji (Theatres) pamoja na kuzuia maambukizi ya
Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,"anaongeza.

Akielezea kuhusu tuzo, Dk. Kyaruzi anasema ya Rais Kikwete inatokana

na jitihada mbalimbali, na wanatambua kwa kuipa  kipaumbele sekta ya
afya.

Alipoingia madarakani mwaka 2005, bajeti ya sekta ya afya ilikuwa ya

sita, hivi sasa
ni ya tatu ikifuatiwa na miundombinu na elimu ambapo sekta hizi zote
zinategemeana huku afya ya mama na mtoto ni ya kwanza katika vipaumbele vya
Wizara ya Afya.

"Rais ameunga mkono kampeni ya malaria haikubaliki ili

kulinda afya ya mama wajawazito na watoto wachanga, katika kufanikisha
malengo ya kupunguza vifo vya mama na mtoto duniani, Umoja wa mataifa
uliunda tume ya kuratibu taarifa na uwajibikaji juu ya afya ya mama na
mtoto na kumteua Rais Kikwete  kuwa mwenyekiti mwenza  wa tume hii
pamoja na Waziri Mkuu wa
Canada .

"Hii ni heshima kubwa kwa nchi yetu, ni imani kubwa dunia iliyonayo

juu yetu watanzania. Tuzo hii kwake ni ujumbe kwa jumuia ya kimataifa
kwamba na sisi watanzania tunamwamini Rais Wetu,  tunamuunga mkono,"anaongeza.

Anaitaja tuzo ya Rais Mstaafu Mwinyi, kwamba imetokana na kazi nzuri

hasa  kupinga
maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na jitihada zake za mara kwa mara kuunga
mkono  matembezi ya hisani, kuwezesha upatikanaji wa fedha kusaidia watoto
wenye matatizo ya moyo  na saratani ili wapate matibabu ndani na nje ya
nchi.


Mkapa naye anapewa tuzo kwa kazi nzuri anayoifanya kupitia taasisi

yake ambapo Dk. Kyaruzi anasema, anafana kazi kubwa  kujali afya ya
mama na mtoto.

Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), nayo ni chanzo kikuu

kilichosababisha Mama Salma kupata tuzo kutoka madaktari hao.


Kwa mujibu wadk. Kyaruzi, Mengi anapata tuzo kutokana na utayari wake

kuisaidia jamii,
kupitia vyombo vyake, Taasisi ya Madaktari Wanawake (MEWATA) wamefanya
kazi kubwa
ya kuokoa maisha ya wakina mama kutokana na Saratani ya Matiti na Shingo ya
Kizazi.

Tuzo za kitaaluma zinaenda kwa Dk. Faraja Nipwapwacha, Daktari

Msaidizi , wa Kituo cha afya Kilimarondo mkoani Lindi , wilaya ya
Nachingwea, ambaye kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita hajapata
vifo vinavyotokana na uzazi.

"Uwezo wake wa kujituma na tabia yake ya kufanya

maamuzi sahihi kwa wakati na haraka katika kuokoa maisha
ya mama na mtoto, ametoa hamasa kubwa kwamba tunaweza kuzuia vifo
vinavyotokana na ujauzito ata sehemu nyingine nchini,"anasema Dk. Kyaruzi.

Anasema THPI inatambua kazi kubwa inayofanywa na wauguzi nchini katika

jitihada za
kuboresha afya ya mama na mtoto kupitia.

Muuguzi  ambaye amependekezwa na wauguzi wenzake kupitia chama chao

kitaifa cha TANNA ni Elia  Mwumbui kutoka kijiji cha Matongo,
kitongoji cha Kimbiji, wilaya ya Ikungi, tarafa ya Ikungi Singida
vijijini kwa kuwa mfano wa wakina baba wanaoshiriki kusindikiza
kliniki wake zao wajawazito.

Anasema lengo ni kuhamasisha kuhusu afyaya mama na mtoto, kwani

wanaamini wajawazito na watoto wao wakiwa salama, taifa litakuwa
salama na
tutajihakikishia ustawi kama Taifa.

"Namshukuru  Dk. Mary Nagu, Waziri wa Uwezeshaji na

Uwekezaji  kwa kutuunga mkono, Dk. Asha Rose
Migiro kwa kuwa mlezi wa vijana wa THPI, taasisi na watu binafsi
walioonyesha nia ya kusaidia sehemu ya kampeni hii ya Saidia Mama Mjamzito
ajifungue salama inayoendeshwa na taasisi yetu ya THPI,"anaongeza.


Dk. Kyaruzi anasema wana mradi wa kujenga uwezo kwa vituo vya afya

katika kuzuia maambukizi ya Virusi vya  UKIMWI kutoka kwa mama kwenda
kwa mtoto katika Wilaya za Iringa Vijijini , Wangig'ombe na Mpanda na
umeandaliwa kwa weledi wa hali ya juu na
mshauri mkuu akiwa Dk. David Urassa, unasubiri uwezeshaji wa fedha ili
utekelezaji uanze.

"Pia mradi wa ujenzi jengo la akina mama wajawazito kata ya Ikindilo, kituo

cha afya Ikindilo wilaya ya Itilima mkoa mpya wa Simiyu nao unasubiri
uwezeshaji wa
fedha kuutekeleza,"anamaliza.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...