Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, November 23, 2013

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF, WAJITOSA RASMI UDHAMINI WA MICHEZO


 Meneja wa LEPF Kanda ya Dar es Salaam, Amina Kassim, akikabidhi jezi kwa M-Kiti wa TUSA, Asnati Chagu. Kushoto ni mweka hazina wa TUSA, Yusuph Singo na Kulia ni Afisa Masiko wa LAPF, Rehema Mkamba.
***************************************
*MFUKO WA PENSHENI WA LAPF UMEJIKITA RASMI KATIKA UDHAMINI WA MICHEZO

KWA KUANZA RASMI NA  MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO KWA
CHAMA CHA MICHEZO VYUO VIKUU TANZANIA (TUSA)
Mfuko wa pensheni wa LAPF ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii nchini Tanzania
wenye makao makuu yake Mjini Dodoma, leo umekabidhi vifaa vya michezo
vyenye thamani ya shilingi milioni tano (5,000,000/=) kwa Chama cha
michezo cha Vyuo Vikuu vya Tanzania TUSA,  kwa ajili ya mashindano ya
TUSA yatakayofanyika mjini Dodoma kuanzia tarehe 10 - 17 Desemba,
2013.
Sherehe fupi ya makabidhiano, imefanyika leo, katika Ofisi za LAPF,
zilizoko Milenium Towers hapa jijini Dar es Salaam, ambapo Meneja wa
LAPF Kanda ya Dar es Salaa, Bibi Amina Kassim, amesema Mfuko wa
Pensheni wa LAPF umekuwa pia ukitoa misaada mbali mbali ya kijamii
katika kusaidia sekta mbali mbali kama elimu, hospitali, vituo vya
kulea watoto yatima na pia katika sekta ya michezo kusaidia kuinua
michezo nchini.
Bibi Kassim amesema, hii ni mara ya tatu kwa LAPF kudhamini mashindano
kwa mara ya kwanza LAPF ilidhamini mashindano ya mwaka 2011 na 2012,
ambapo LAPF imetoa vifaa hivi kwa kutambua umuhimu wa wanafunzi wa
taasisis hizo kama wanachama wetu watarajiwa.
Amesema kufuatia LAPF kuwa Mfuko bora wa Pensheni kwa kudhihirishwa
kwa tuzo iliyotolewa na Msimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii SSRA
kuwa LAPF kuwa ni  Mfuko wa Pensheni unakua kwa kasi Zaidi nchini.
Na kitendo cha LAPF kuwa imekuwa ikipata tuzo kutoka kwa bodi ya
wahasibu nchini NBAA kwa kuwa Mfuko wenye Hesabu Bora za mwaka kwa
miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2008, 2009, 2010 na 2011, LAPF
sasa imeamua kujikita kudhamini michezi, ili kurudisha kwa jamii,
sehemu ya mafanikio hayo.
Akishukuru kupata vifaa hivyo, Mwenyekiti wa TUSA Taifa,  Asnati Chagu
aliishukuru LAPF kwa msaada huo, na kusema umekuja wakati muafaka, ila
pia akaomba wafadhili wengine wazidi kujitokeza ili kufanikisha
michuona hiyo.
Amesema msaada huoi wa jezi ni moja tuu ya mahitaji, lakini bado kuna
mahitaji mengine yanahitajika vikiwemo vikombe na zawadi kwa washindi
mbalimbali

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...